Sharifa Marira
TOFAUTI ya Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad imetajwa
kuwa ni utendaji kazi wao, huku mmoja akitajwa mwenye kinyongo na mwingine mpenda
umoja.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya
Vijana (JUVICUF) Khomein Rwihula alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na
JAMBO LEO kuhusu mgogoro wa pande mbili uliopo katika chama hicho.
Rwihula ambaye pia aliwahi kugombea
Ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita,
alisema Lipumba anaendelea kufanya kazi ya kukijenga chama, hana kinyongo na
mwanachama yeyote tofauti na Maalim Seif ambaye hafanyi kazi wala hafiki
ofisini.
“Profesa Lipumba ni kiongozi wa mfano, yeye
anafanya kazi tu, amejitahidi kumuita ofisini Maalim Seif ili aje ampangie
majukumu ya kazi za kukijenga chama kwa mujibu wa katiba, lakini hajatokea,kazi
yake ni kushughulika na kufukuza watu huko Zanzibar,’’alisema Rwihula.
Alisema Maalim Seif anapaswa kumuelewa
Lipumba kuwa ana dhamira ya dhati ya kukijenga chama kwa kuwa hajatangaza
mapambano na mtu isipokuwa amewaita kufanya kazi lakini hawajatokea.
Akizungumzia suala la CUF ya Maalim Seif
kutangaza kwenda mahakamani kutafuta haki, alisema wanasita kutekeleza jambo hilo kwa kuwa wamejua watakwama
kutokana na Lipumba kutambulika kisheria.
“Tunajua kuwa sasa wanahangaika hawajui
la kufanya kwa sababu wakiwaza kwenda mahakamani wameshajua kuwa itakula kwao,
kwani katiba waliyoiandika wenyewe itawamaliza.’’
Alisema kinachotakiwa kufanywa na Maalim
Seif na wafuasi wake ni kukubali kukaa meza moja ya mazungumzo na Profesa
Lipumba ili waendeleze majukumu ya chama kama ambavyo anafanya kwa kupita
kufanya mikutano mikoani.
0 comments:
Post a Comment