Mwandishi Wetu
Abdul-Razaq Badru |
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
imetangaza siku 90 kuanzia jana ikitoa nafasi kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka
wa masomo 2016/17 kukata rufaa kwa njia ya mtandao, wakiona hawajaridhsihwa na
matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB
Abdul-Razaq Badru, ilisema Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao
kuanzia jana na itaendelea kupokea hadi Januari 31.
Serikali imetenga Sh bilioni 483 za mikopo kwa wanafunzi
119,012, kati yao 93,295 ni wanaondelea
na masomo na 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183
wa mwaka wa kwanza wamepata mikopo.
“Wanachotakiwa kufanya ni kulipa Sh 10,000 kwa njia ya
M-Pesa na kuingia kwenye mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Ofisa
Mikopo wa Chuo husika ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo kwa barua kwa
ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” alisema Badru.
Katika taarifa yake inayopatikana pia kwenye tovuti ya
HESLB Badru aliongeza kuwa Bodi yake haitapokea wala kuzifanyia kazi fomu za
rufaa zitazowasilishwa na wanafunzi bila kupitia kwa maofisa mikopo wa vyuo husika.
0 comments:
Post a Comment