Suleiman Msuya
Tumaini Makene |
WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), wamechagua wenzao watano watakaowakilisha kundi la wabunge
kwenye Kamati Kuu ya Chama hicho.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Chama
hicho, Tumaini Makene ilisema wabunge hao wamechaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya
7.7.14 (g) ya Katiba ya Chadema inayotoa nafasi tano za kuchagua wajumbe wa Kamati
Kuu kuwakilisha kundi hilo.
Alitaja wabunge waliochaguliwa kuwa ni
Tundu Lissu (Singida Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Esther Bulaya
(Bunda Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na wa Viti Maalumu Mariam Msabaha.
Aidha, alisema Chadema imetuma ujumbe wa
viongozi wa Kamati Kuu Dodoma kuzungumza na wabunge wao kuhusu Muswada wa
Huduma za Vyombo vya Habari ambao unatarajiwa kuwasilishwa bungeni na Serikali.
Alitaja wajumbe wa Kamati Kuu waliokwenda
Dodoma kuwa ni Makamu Mwenyekiti Bara, Profesa Abdallah Safari, Profesa Mwesiga
Baregu, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick
Sumaye na Arcado Ntagazwa.
0 comments:
Post a Comment