Mery Kitosio, Arusha
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa |
MIFUKO ya
hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wameungana kujenga
kiwanda cha sukari eneo la Mkulazi mkoani Morogoro ili kukabiliana na tatizo la
sukari nchini.
Akizungumza kwenye
ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa NSSF ulioanza jijini hapa jana, Waziri
Mkuu Kasimu Majaliwa alisema amefurahishwa na uamuzi wa taasisi hizo kujenga kiwanda ili kukabiliana na tatizo hilo.
Majaliwa alisema
kitendo kilichofanywa na mashirika hayo ni
cha kuungwa mkono na mashirika mengine kuiunga mkono Serikali kuifanya Tanzania
kuwa nchi ya viwanda.
Alisema tathimini
ya Tanzania ya kuwa na mahitaji ya zaidi ya tani 400,000 za sukari si sahii na
hivyo kuiagiza Bodi ya Sukari kufanya tathimini mpya ya mahitaji ya sukari, ili
viwanda viwe na tathimini ya kiwango cha uzalishaji.
"Nitoe mwito
kwa kampuni na taasisi kuiga mfano wa NSSF na PPF kuunganisha nguvu katika
utekelezaji wa agizo la kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda, ili kukuza uchumi wa
nchi yetu," alisema Majaliwa.
Awali Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kua shirika hilo limejizatiti
kuwekeza kwenye sekta ya viwanda ili kuviwezesha kujiendesha kwa ufanisi na
kuleta tija kwa wananchi.
Profesa alisema wameitika
mwito wa Rais kuijenga Tanzania ya viwanda kwa kuungana na PPF kujenga kiwanda
hicho.
"Tunatarajia
kujenga kiwanda hiki ambacho kitapunguza tatizo la sukari lakini pia kitatoa
ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza idadi ya wanachama,"
aliongeza Mkurugenzi.
Alihitimisha kwa
kuwataka waajiri kuharakisha kuwasilisha makato ya waajiriwa wao kwa mujibu,
kwani ucheleweshaji ni moja ya changamoto zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment