Washauriwa kutumia matrekta ya Sonalika


Suleiman Msuya 


WATANZANIA wameshauriwa kutumia matrekta mapya aina Sonalika HP 120 kwenye kilimo kwani yanamudu kutumika kwenye ardhi ya aina yoyote nchini kwa kuwa ni imara.

Ushauri huo ulitolewa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kampuni za Quality Group, Arif Sheikh, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa matrekta hayo yaliyotengezwa na kampuni ya International Tractors Limited ya India.

Alisema kwa muda mrefu sasa wakulima wamekuwa wakitumia matrekta yenye nguvu za HP 20 hadi 90 hivyo ujio wa matrekta haya ya nguvu za HP 120 utakomboa wakulima wengi waliokuwa wanalalamika.

Mkurugenzi huyo wa Quality Group yenye pia kampuni tanzu ya Farmequip Tanzania Ltd inayouza matrekta hayo alisema wamejipanga kuhakikisha wakulima wa Tanzania wanayapata ili kukuza kilimo chao.

Sheikh alisema ni jambo la faraja wao kuandaa mkutano na uzinduzi wa matrekta hayo ambapo nchi 26 zimeshiriki.

"Napenda kutumia nafasi hii kuomba na kushauri wakulima wa Tanzania kutumia matrekta haya kwa kuwa ni mazuri yenye nguvu ya kumudu ardhi yoyote," alisema.

Alisema Farmequip imejipanga kufikia watu wote wanaohitaji matrekta hayo hivyo wawasiliane nao.

Rais wa International Business (IB), Gauranv Saxena alisema kampuni yao imejipanga kuhakikisha inakamata soko la matrekta duniani.

Saxena alisema kampuni yao kila kukicha inabuni mbinu mpya za kuboresha matrekta ili kukidhi mahitaji ya wakala na wateja wao.

Alisema matrekta hayo ni miongoni mwa bora yaliyopata kutengenezwa duniani hivyo anaamini watumiaji watafurahia mara yatakapoingia sokoni.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Deepak Mittal alisema wanafanya biashara na nchi 80 duniani huku Afrika ikiwa mteja wao mkubwa.

Mittal alisema matrekta yao yanauzwa Amerika Kusini na Kaskazini, Ulaya, Asia, Mashariki ya Kati, Afrika na India.

Meneja Mkuu wa International Tractors Limited, Gurmeet Dang alisema mipango yao hadi mwaka 2020 ni kuuza matrekta 10,000 Afrika ambapo sasa wanauza 5,000 tu.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Laptop City

Tangazo