Leonce Zimbandu
Rita Ramalho |
BENKI ya Dunia imeitaja Mauritania kuongoza kufanya biashara za
kimataifa kati ya nchi 49 zilizo kwenye ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara,
huku Kenya ikifuatia kwa kufanya vizuri kwa miaka miwili mfululizo.
Meneja wa Mradi wa Biashara wa Benki hiyo, Rita Ramalho aliitaja nchi
hiyo kuongoza wakati wa kuzindua ripoti ya mwaka ya biashara iliyofanyika Dar
es Salaam jana.
Alisema ripoti hiyo imezingatia viashiria vya kukua kwa uchumi katika
nchi husika, ikiwamo Mauritania, ambayo
imefanikiwa katika kulinda wawekezaji na kushughulikia utoaji wa vibali ya ujenzi
kwa mtiririko kwa siku 156 tofauti na siku 183 za Ufaransa na 222 za Austria.
Alisema Kenya kwa mara ya pili mfululizo imefanikiwa kutatua tatizo la
kupata idadi ya vizazi na vifo kwa kufuta ada ya uandikishaji na utoaji vyeti,
kuanzisha mfumo wa habari kwa ajili ya kupata nishati ya umeme ili kupunguza
muda wa mwingiliano.
"Bado jitihada za kufanya biashara kirafiki zinahitajika hasa
kutokana na maboresho thabiti ya kiuchumi katika kanda mbalimbali, ingawa
rekodi ya idadi ya mageuzi imeongezeka kwa asilimia 14 ikilinganishwa na mwaka jana,
hivyo serikali zinapaswa kuweka msukumo katika mageuzi ya kiuchumi,” alisema.
Ripoti ya mwaka huu ilipokea kwa mara ya kwanza maombi ya Somalia na
kufikisha nchi wanachama 190 ambayo kiuchumi hivi sasa inashika nafasi 190.
Ripoti ya biashara ya mwaka huu ilijikita kwenye viashiria vitatu ambavyo ni kuanzisha biashara, kusajili mali na kutekeleza mikataba iliyokubaliwa kimataifa kwa ajili ya kuboresha biashara na kuleta mageuzi ya kiuchumi.
Ripoti ya biashara ya mwaka huu ilijikita kwenye viashiria vitatu ambavyo ni kuanzisha biashara, kusajili mali na kutekeleza mikataba iliyokubaliwa kimataifa kwa ajili ya kuboresha biashara na kuleta mageuzi ya kiuchumi.
Aidha, ripoti hiyo ilisema hatua za ziada zinahitajika kwa ajili ya kukomboa
wanawake kwa kusajili biashara zao katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, zikiwamo
Cameroon, Benin na Guinea-Bissau.
0 comments:
Post a Comment