Warioba Igombe, Morogoro
Hamis Mabura hospitalini |
Diwani wa Kata ya Koloro (CCM), Erigius Mbena alithibitisha tukio hilo akisema wakulima hao walipatwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Korelo na Lukange na sasa wamelazwa katika kituo cha afya cha kata hiyo.
Inadaiwa kuwa wafugaji wasiojulikana walikotoka, walifika katika vijiji hivyo wakiwa na mifungo ambayo inaonekana kuwa kero kwa wananchi wa maeneo hayo kwani mifugo hiyo imekuwa ikilishwa kwenye mashamba ya watu.
“Ni kweli kuwa wakulima zaidi ya watu 12 katika kata yangu wamejeruhiwa baada ya kukatwakatwa kwa mapanga na wafugaji wa jamii ya Wamasai kutokana na wakulima hao kuzuia mifugo iliyokuwa ikilishwa mazao yao shambani,” alisema Mbena.
Mbena alisema kuwa wakulima hao wamejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili na kulazwa katika kituo cha afya cha kata hiyo huku hali zao zikizidi kuwa mbaya.
Diwani huyo alieleza kusikitishwa na Serikali ya wilaya hiyo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushindwa kutatua mgogoro huo licha ya mara kadhaa kuwafikishia taarifa wahusika.
Alieleza vijiji vya kata hiyo kwa muda mrefu vimekuwa vikimilikiwa na wakulima ambao wamekuwa wakilima mazao mbalimbali ambapo alieleza amesikitishwa na kitendo wafugaji kuvamia eneo hilo wakiwa na kundi kubwa la mifugu.
Mkazi wa kijiji hicho, Juma Omary amemuomba Rais Magufuli kusaidia kumaliza tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wafugaji hao ili warudi walipotoka kwani wamekuwa wakiwatishia maisha kwa kigezo kuwa wao ni masikini.
Mgogoro huu ulioambanana na fujo na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa umekuja siku chache ambapo mkuu wa mkoa Stephen Kebwe kukaririwa na vyombo vya habari hakisema kwa sasa amani imetawala Morogoro.
0 comments:
Post a Comment