Emeresiana Athanas
SERIKALI imezisisitizia halmashauri zote nchini kutenga
asilimia tano ya mapato yake kwa ajili ya kuwaendeleza vijana.
Pia, imesema itaweka mazingira yanayostahili katika
kuwapatia vijana unafuu wanapojitoa kushiriki katika kilimo.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Florens Turuka wakati wa uzinduzi wa
mkakati wa kuhusisha vijana katika kilimo.
Dk. Turuka alisema kuwa hadi sasa Serikali inaendelea
kukamilisha mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo wa mwaka 2016/17. Alisema
mpango huo utatoa fursa kwa vijana kushiriki katika kilimo.
"Lengo la Serikali ni kuhakikisha nchi inapata
maendeleo yatakayoletwa na kilimo, ambapo vijana ndio wenye nafasi kubwa katika
kuchangia suala hilo," alisema.
Aliongeza kuwa taasisi za kifedha zina jukumu la kutumia fursa ya ushiriki wa vijana katika
kuwania katika kilimo na kuwataka vijana kuwa mstari wa mbele katika mageuzi
kwenye sekta ya kilimo.
0 comments:
Post a Comment