Enlesy Mbegalo
Profesa Innocent Ngalinda |
WAKUSANYA takwimu wametakiwa kutoa takwimu sahihi ili
kuiwezesha Serikali kupanga mipango yake.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo cha
Takwimu Mashariki mwa Afrika, Profesa Innocent Ngalinda alipozungumza na
waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya wakusanya takwimu yaliyoanza Oktoba 17.
Profesa Ngalinda alisema ili kuhakikisha ubora wa takwimu
unazingatiwa na kulingana na matakwa ya kiutendaji ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), ni lazima anayefanya awe amepitia chuo hicho.
“Takwimu ni taaluma kama nyingine ukikosea Serikali
itashindwa kupanga maendeleo ya baadaye na ili kuondokana na mazoea ya
ukusanyaji taarifa, tumeaza kutoa mafunzo hayo ili kupunguza gharama za
ukusanya takwimu,” alisema Profesa Ndalinda.
Alisema mafunzo hayo yaliandaliwa ili kumpa mshiriki
ujuzi katika ukusanyaji takwimu kwenye mazingira mbalimbali kwa ajili ya
kuzichakata na kuwa takwimu rasmi.
“Nashauri umma kuchangamkia fursa ya mafunzo haya kwa
sababu uhitaji wa wakusanya takwimu wenye ujuzi unakua,” alisema.
0 comments:
Post a Comment