Richard Mwangulube, Arusha
TANZANIA imepiga marufuku uingizaji mazao ya migomba
kutoka Msumbiji baada ya nchi hiyo kukumbwa na ugonjwa wa Panama.
Mbali na hatua hiyo pia Tanzania imeweka karantini nchi
nzima kuzuia uingizaji wa mazao hayo.
Haya yalisemwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi, Dk Florence Turuka katika hotuba yake wakati akifungua
mkutano wa watalaamu wa afya ya mimea kutoka nchi za SADC na COMESA iliyosomwa
kwa niaba yake na Cornelius Mkondo Mkurugenzi Msaidizi wa afya ya mimea.
Dk Turuka katika hotuba hiyo alisema Msumbiji inapakana
kwa karibu sana na Tanzania hivyo si jambo jema wananchi kuruhusu
migomba ama mazao ya migomba kutokana na ugonjwa huo hatari.
Katika kuhakikisha mazao ya migomba hayaingii
nchini kutoka Msumbiji, Tanzania imeweka wataalamu wake wa
mimea mpakani na nchi hiyo, viwanja wa ndege na maeneo yote muhimu ili
kuimarisha ukaguzi
Kwa mujibu wa Dk Turuka, Tanzania kwa sasa haiwezi
kusafirisha matunda kwenda Afrika Kusini kutokana na mdudu hatari anayeshambulia
matunda.
Aliwambia washiriki wa mkutano huo kutoka nchi 15 za SADC
na COMESA umuhimu wa kuwa na mikakati ya pamoja kukabiliana na magonjwa ya
mimea katika ukanda huu wa Afrika.
Alisema hakuna nchi itakayokubali kununua matunda ya
Tanzania ili kuepuka ugonjwa huo kuenea kwenye mataifa yao.
0 comments:
Post a Comment