Grace Gurisha
Mahakama ya Kisutu |
HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar
es Salaam, Respecious Mwijage, ameutaka upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya
mashitaka katika kesi ya kusambaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, kabla
ya kuthibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Kesi hiyo inakabili wafuasi wa Chadema na raia wa kigeni na
lengo la mwito wa Hakimu Mwijage ni kumwondoa kwenye orodha mshitakiwa
aliyefariki ndunia.
Mwijage alifikia uamuzi huo jana na kuahirisha kesi hiyo,
baada ya kubaini kuwa katika hati ya mashitaka kuna washitakiwa wanane, wakati kwenye
nyaraka za maelezo ya awali, zinatambulisha washitakiwa saba hali ambayo
alihofia inaweza kuleta matatizo baadaye.
Kutokana na kubainika kwa makosa hayo, mawakili wa
Serikali Grace Komba na Estazia Martin walishindwa kuwasomea washitakiwa
maelezo yao.
Kabla ya Hakimu kutoa tarehe ya washitakiwa hao kusomewa
maelezo hayo, mawakili wa utetezi, Tundu Lissu na Peter Kibatala walikubaliana
na uamuzi huo wa kwenda kubadilishwa hati ya mashitaka.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi kesho washitakiwa
watakaposomewa maelezo yao. Hatua hiyo inatokana na Jose Nimi (51) raia wa
Ufaransa kufariki dunia.
Washitakiwa wengine ni Mashinda Mtei (49) wa Tengeru,
Arusha, Julius Mwita (40) wa Magomeni, Dar es Salaam, Frederick Fussi (25) wa
Mbezi, Dar es Salaam, Julius Matei (45) wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji
wa Keko na Anisa Rulanyan (41) wa Kawe.
Katika kesi hiyo ya mwaka jana yenye mashitaka matatu wanakabiliwa
na madai ya kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua
hazijathibitishwa.
Ilidaiwa kuwa Matei na Nimi, Oktoba 26 mwaka jana wakiwa kwenye
hoteli ya King, Kinondoni wakiwa na hati za kusafiria namba A1532119, 930879 na
M 27687807 walijiingiza kwenye ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais
ya uchaguzi wa mwaka jana ya Chadema bila kibali.
Mashitaka la ya tatu yanamkabili Matei peke yake mwenye
hati ya kusafirilia namba A1532119 ambaye inadaiwa akiwa Dar es Salaam
alijihusisha na biashara kwenye Saccos ya Wanama bila kibali.
0 comments:
Post a Comment