Celina Mathew
Dk. Charles Msonde |
SERIKALI imetangaza matokeo ya mtihani
wa Taifa wa darasa la saba uliofanyika Septemba 7 na 8 huku shule ya msingi ya Kwema
ya mkoani Shinyanga ikiongoza kwa kutoa watahiniwa saba bora kitaifa kati ya Kumi
Bora na kuongoza kitaifa.
Akitangaza matokeo hayo jana Dar es
Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania, Dk Charles Msonde
alisema watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa
kupata alama 100 au zaidi ya alama 250.
Alisema idadi hiyo ya watahimiwa
waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36 na kwamba kati yao, wasichana ni 283,751
sawa na asilimia 67.59 na wavulana ni 271,540 sawa na asilimia 73.50 ikilinganishwa
na mwaka jana, ambapo watahiniwa walikuwa asilimia 67.84 hivyo ongezeko la
asilimia 2.52 ya ufaulu.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa ufaulu
katika masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06
na 14.76 ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa upande wa masomo ya Kiswahili,
Hisabati na Kiingereza, Dk Msonde alisema ufaulu umeshuka kwa kati ya asilimia
0.39 na 12.51 ikilinganishwa na mwaka jana.
Alisema watahiniwa wamefaulu zaidi
Kiswahili unaofikia asilimia 76.81 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini
zaidi ni Kiingereza ambayo ni asilimia 36.05.
Wahitimu
10 bora
Alitaja wanafunzi kumi bora kuwa ni Japhet
Stephano (Kwema, Shinyanga), Jamal Athuman, Enock Bundala, Justina Gerald (Tusiime,
Dar), Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine (Kwema), Isaac Issac (Kwema),
Daniel Kitundu (Kwema), Benjamin Shabu (Kwema) na Azad Ayatullah wa (Kaizirege,
Kagera).
Wasichana
10 bora
Kwa wasichana 10 bora aliyeongoza ni
Justina Gerald, akifuatiwa na Danielle Onditi wote wa Tusiime, huku wa tatu
akiwa ni Linda Mtapima (Kaizirege).
Wengine ni Cecilia Kenene (Mugini, Mwanza),
Magdalena Deogratius (Rocked Hill, Shinyanga), Asnath Lemanya (Tusiime), Fatuma
Singili (Rocken Hill).
Pia Ashura Makoba (Kaizirege), Rachel
Ntitu (Fountain Of Joy, Dar) na Irene Mwijage (Atlas, Dar).
Wavulana
10 bora
Wavulana 10 bora ni Japheth Stephano (Kwema),
Jamal (Kwema), Enock Bundala (Kwema), Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine
(Kwema), Isaac Issac (Kwema), Daniel Katundu (Kwema), Benjamin (Kwema), Azad
Ayatullah (Kaizirege) na Beneth Hango (Kwema).
Shule
10 bora
Shule zilizo kwenye kundi la 10 bora
kitaifa ni Kwema, Rocken Hill, Mugini, Fountain of Joy, Tusiime, Mudio Islamic (Kilimanjaro),
Atlas, St. Achileus (Kagera), Gift Skillfull (Dar) na Carmel ya Morogoro.
Shule
10 za mwisho
Shule 10 zilizoshika mkia ni Mgata (Morogoro),
Kitengu (Morogoro), Lumba Chini (Morogoro), Zege (Tanga), Kilole (Tanga), Magunga
(Morogoro), Nchinila (Manyara), Mwabalebi (Simiyu), Ilorienito (Arusha) na
Chohero ya Morogoro.
Mikoa
10 bora
Dk Msonde aliitaja mikoa 10 iliyiofanya
vizuri kitaifa kuwa ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro,
Arusha, Njombe na Tabora.
Halmashauri
10 bora
Halmashauri zilzofanya vizuri kitaifa
alizitaja kuwa ni Mpanda (Katavi), Geita Mjini (Geita), Arusha Mjini, Mafinga Mjini
(Iringa), Chato (Geita), Mwanza Mjini, Moshi Mjini (Kilimanjaro), Makambako Mjini
(Njombe), Ilemela (Mwanza) na Hai (Kilimanjaro).
Hata hivyo, Dk Msonde alisema Baraza
hilo liliwafutia mitihani wanafunzi 238 waliobainika kufanya udanganyifu kwa
mujibu wa kifungu 32(2)(b) cha kanuni za mitihani.
Aidha, Baraza lilishauri mamlaka husika
kuwachukulia hatua waliohusika kwa namna moja au nyingine kusababisha
udanganyifu huo kwa mujibu wa kanuni za utumishi na sheria za nchi.
0 comments:
Post a Comment