* Watakaotuhumiwa rushwa kufutwa kazi
* Haijalishi
wameshinda au kushindwa kesi
Mary
Kitosio, Arusha
Jaji Mkuu Mohamed Chande |
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed
Chande, ameshauri mahakimu watakaoshitakiwa kwa rushwa waondolewe kazini.
Akizungumza na majaji wafawidhi
wa Mahakama Kuu na wengine jijini hapa jana, Jaji Mkuu Chande alitoa ushauri
huo kwa Tume ya Utumishi wa Mahakama, akiwataka mahakimu kusimamia maadili na atakayebainika
amepokea rushwa ataondolewa kazini.
Alisema idara nyingi za Mahakama zinaonekana kulalamikiwa
na wananchi kwa rushwa na watakaobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Mahakimu wa ngazi za chini wamekuwa wakilalamikiwa na
wananchi kwa kutosimamia maadili, nimeshatoa ushauri kwa Tume, kwamba hakimu atakayeshitakiwa
kwa rushwa ataondolewa kazini hata kama atashinda kesi,” alionya Jaji Mkuu Chande.
Jaji Mkuu pia
aliwataka majaji kuja na mikakati ya kuhakikisha kasi ya kupunguza kesi
mahakamani inaongezeka hasa za muda mrefu ili kupunguza malalamiko yanayotokana
na kuchelewa kutoa hukumu na kutopatikana kwa nakala za hukumu kwa wakati.
Pia Jaji Mkuu aliwataka
majaji kusimamia maadili ndani ya taasisi hiyo ili kurejesha imani ya wananchi
kwa Mahakama yao.
Katika hatua
nyingine, Jaji Mkuu aliwapongeza majaji na majaji wafawidhi kwa kumaliza vizuri
kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu nchini pamoja na kutenga
muda wa kujadili changamoto zilizotokana na kesi hizo.
Alisema majaji hao walijitolea kusikiliza kesi hizo na nyingi kuzitolea hukumu kwa kipindi kifupi licha ya chache kubaki mahakamani.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu Chande, jumla ya kesi 53 za ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana zilifunguliwa Mahakama Kuu kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza.

Kanda nyingine
ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga na Tanga ambapo kati ya hizo, 31 zilimalizika
katika hatua za awali na 22 ziliendelea na hadi sasa 19 zimemalizika na tatu
bado ziko mahakamani.
Hata hivyo, kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika mahakama mbalimbali za mahakimu wakazi nchini katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Zaidi ya
asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika
wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika pia.
Katika mkutano huo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Ferdinand Wambali alisema Watanzania wana imani na Mahakama, hivyo ni muhimu majaji na mahakimu wakatenda haki kwa wote na wakati wote.
0 comments:
Post a Comment