Mwandishi Wetu, Dodoma
Mohamed Mchengerwa |
SHILINGI
milioni 800 ndizo zilizotumika kukarabati miundombinu katib ya Sh bilioni 5
zilziotolewa kwa ajili ya waathirika wa tetemeko mkoani Kagera, imeelezwa.
Hayo
yalisemwa juzi mjini hapa na Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria, Mohamed
Mchengerwa (CCM) alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano kati
ya Kamati hiyo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama uliokuwa ukipokea taarifa ya madhara ya tetemeko
hilo.
Alisema
Serikali inaendelea kusaidia waathirika hao na kwa sasa wanafunzi wa sekondari ya
Ihungo wamehamishwa shule ya Mwani ili kuendelea na masomo.
Mchengerwa
alisema taarifa ambayo Kamati hiyo ilipokea ilisema wagonjwa 440 walio hospitalini
wanaendelea kupata matibabu na sita wamefariki dunia.
“Wagonjwa
sita wamefariki dunia hivyo idadi ya vifo kuongezeka kutoka 17 hadi 23, wananchi
wanaendelea kupata huduma ukiwamo uboreshaji wa miundombinu na wanajeshi wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) 96 wako Kagera kulinda usalama,’’ alisema
Mchengerwa.
Alisema
inatakiwa miaka miwili au mitatu mkoa huo kukaa sawa kutokana na maeneo mengi
kuathirika na ukarabati unafanyika taratibu.
“Kamati
imeshauri Serikali isimamie afya na usalama wa wananchi waliopatwa na tetemeko,
kuendelea kuratibu suala hilo kwa kushirikiana na wahisani; wataalamu wa ndani
watumike kufanya utafiti katika maeneo ya bonde la ufa kabla ya maafa kutokea,’’
alisema Mchengerwa.
Pia
Kamati iliiomba Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tetemeko na kujenga
nyumba imara zinazostahimili mtikisiko, kuboresha kitengo cha maafa na
kuanzisha vituo vya kitaifa vyenye vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majanga.
Kuhusu
Serikali kuhamia Dodoma, Kamati ilishauri kuwepo sheria maalumu kusisitiza
jambo hilo na kuongeza nguvu za kusimamia Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu
(CDA) ambayo imeonekana kuwa na urasimu mkubwa katika upangaji ardhi.
“Serikali
imeahidi kuhakikisha CDA haiendelezi urasimu katika upangaji na ugawaji ardhi
kwa matumizi mbalimbali, kwani itaanza kutumia mfumo wa elektroniki katika
ununuzi wa ardhi,‘’ alisema.
Alisema
hadi sasa wizara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi
wameshapewa maeneo kwa ajili ya kujenga ofisi na watumishi wa umma, wabunge na
maofisa wengine wataanza kupewa maeneo.
0 comments:
Post a Comment