Abraham Ntambara
Shaka Hamdu Shaka |
UMOJA wa Vijana
wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umesema taratibu zilizotumika
kumpata meya mpya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sita kuwa zilikuwa sahihi
na zilifuata miongozo ya kanuni, sheria na Katiba.
Kaimu Katibu Mkuu, Shaka Hamdu Shaka,
alisema hayo wakati akizungumza mwishoni mwa juma na mwandishi wa habari hii.
“Tunaamini kwamba
kulikuwa na wasimamizi wazuri wa sheria, kanuni na taratibu, hivyo ni imani yetu
kwamba yote yalifanyika kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi,”alisema
Shaka.
Shaka aliwataka wapinzani
(Ukawa) wakubali kwamba walishindwa kadhalika wao bado ni wachanga kisiasa ikilinganishwa
na CCM.
Aidha aliwataka Ukawa kuacha visingizio kwa kuwa walishindwa
kihalali na malalamiko yao hayana mashiko.
Aliwataka kujua kuwa uchaguzi umemalizika hivyo baada ya
uchaguzi kuna maisha mengine alisema pia wananchi wa Kinondoni washikamane na
washirikiane kwa pamoja kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa halimashauri yao.
Kwa upande mwingiene Shaka alisema Ushindi katika
uchaguzi wa Kinondoni ni kiashiria kuwa kazi ndiyo imeanza ya kuelekea katika
uchaguzi wa serikali za mitaa ujao wa mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Alisema pia hiyo inamanisha kwamba tathimini ya uchaguzi
mkuu uliopita ambapo walifanya makosa na kupelekea kupoteza baadhi ya Manispaa imekwishaanza
kufanyiwa kazi na matunda yameshaanza kuonekana.
Shaka aliongeza kwamba wataendelea kujisahihisha
kulingana na makosa waliyoyafanya ambapo hiyo ni mikakati ya kichama ili
kuhakikisha kwamba hawarejei tena makosa ambayo yakawaghalimu.
Aidha alisema kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli
umeongeza imani kubwa ya wananchi kwa chama chao ambapo alibainisha kuwa
watajitahidi kuwa karibu na wananchi hao ili iwe rahisi kupata ushindi bila
upinzani katika uchaguzi ujao.
0 comments:
Post a Comment