Celina Mathew
Profesa Makame Mbarawa |
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amezindua Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) na
kushauri Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo asiwe mzawa wa nchini.
Aliwataja watendaji hao kuwa ni Stella
Mwanansao, Dk Ubena John, Dk Jasson Bagonza, Fatma Bakari, Khadija Shaaban na
Leonard Kitoke.
Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati
akizindua Bodi mpya ya Shirika hilo yenye wajumbe sita huku nafasi ya Mtendaji
Mkuu ikiwa bado wazi, alisema watu 207 walijitokeza kuwania nafasi hiyo.
Profesa Mbarawa alisema alikuwa akiuliza
watu ili kupata maoni yao kuhusu mtendaji huyo atoke wapi na kwamba aliamua
kuwa asiwe mzawa wa nchini, bali awe wa nje kutokana na kuwa kwa miaka mingi
wazawa wamekuwa wakitumia shirika hilo vibaya.
"Tuliuliza Mtendaji Mkuu atoke wapi
mimi nikaamua atoke nje ambaye hajui hata kupiga muhuri lakini suala kubwa
azalishe fedha maana serikali inataka fedha na si kitu kingine lengo likiwa ni
kuona shirika linasonga mbele kiuchumi," alisema.
Alisema endapo Mtendaji huyo atapatikana
na kulichezea shirika kama waliopita, ataendelea kubadilisha hata kama atakuwa hajamaliza
mwaka hadi apate kile anachokihitaji ambacho ni ukusanyaji mzuri wa mapato.
"Fedha zipo Posta tena nyingi,
lakini hazionekani, haijafungwa mkono bali kulikuwa na watendaji wabovu kipindi
kilichopita, ambapo mwaka jana kulitokea jambo ambalo halikuwa zuri la viwanja
vitatu vya shirika kuuzwa kinyemela na baada ya kugundua tulifanyia kazi japo Bodi
ilikuwa haijui," alisema.
Aliongeza kuwa katika shirika hilo
kulikuwa na watu wanajifanya wajanja na kuahidi kuwa atahakikisha
anawawajibisha, hivyo kuwataka kufikiria zaidi na kuachana na utendaji wa
zamani kwa kutumia fursa zilizopo ili mafanikio yaweze kupatikana.
Aidha, aliahidi kulipa madeni ambayo TPC
inaidai Serikali na kutoa mwaka mmoja kwa shirika hilo kuhakikisha linafungua
kituo cha huduma kwa lengo la kufanya kazi kimaadili na kwa weledi.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali
mstaafu Dk Harun Kondo alisema kwa sasa shirika litakuwa na historia nzuri
kutokana na kuwa wajumbe walioteuliwa ni watendakazi wazuri huku akikiri kuwa
changamoto ya awali iliyokuwapo ilisababishwa na watendaji waliopita.
0 comments:
Post a Comment