Immaculate Ruzika
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa
Jumanne Maghembe ameibadili Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utalii cha Taifa kuwa
Bodi ya Utendaji.
Akizungumza juzi katika ziara yake chuoni
hapo, alisema amebadili Bodi hiyo ili kuboresha utendaji wa chuo hicho.
“Kuwa Bodi ya Ushauri hakutoshi, sasa
kuanzia leo naibadili kuwa Bodi ya Utendaji
ambayo licha ya kushauri, lakini pia itakuwa ikifanyia kazi yale inayoshauri
kwa kuchukua hatua,” alisema.
Profesa Maghembe alisema ili kuboresha chuo
hicho kuwa cha kisasa zaidi, itaundwa Bodi ya Taaluma itakayoshughulika na
mambo ya kitaaluma, ili wanafunzi wanaomaliza chuoni hapo wawe wameiva sawasawa.
Alipendekeza chuo kuanzisha Stashahada ya
Juu ili kuongeza ujuzi kwa wanafunzi wanaomaliza ikiwa ni mkakati wa kuifanya
elimu hiyo kuwa ya kimataifa.
Waziri aliwataka wahadhiri wa chuo hicho
kufanya kazi kwa bidii, ili chuo kiwe miongoni mwa vyuo bora Afrika.
Licha ya kusisitiza hayo, Maghembe
aliwataka viongozi wa chuo kudumisha uafi
wa maeneo ya chuo, hususan jikoni na kwenye majokofu ya kuhifadhi chakula.
‘’Nimepita maeneo mbalimbali nimeona
suala la usafi bado liko chini, hususan jikoni, hiki ni chuo cha kimataifa cha
ukarimu, lazima kiwe safi maeneo yote,’’ alisema Waziri.
Aliongeza kuwa, chuo ni hazina kwa
uchumi wa nchi na kuwa asilimia kubwa ya mapato ya Tanzania yanategemea sekta
ya utalii.
0 comments:
Post a Comment