Mariam Cyprian, Tanga
Profesa Sospeter Muhongo |
SERIKALI za Tanzania na Uganda zimesaini
mkataba wa utekelezaji mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi unaotarajiwa kuanza
hivi karibuni kutoka Ziwa Albert hadi bandari ya Tanga.
Mkataba huo ulisainiwa juzi baada ya
kikao cha siku tatu kati Tanzania na Uganda kilichofanyika mkoani hapa.
Makataba huo ulisainiwa na Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na mwenzakde wa Uganda, Irene
Muloni.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo,
Profesa Muhongo alisema mkataba umegusa maeneo mbali mbali muhimu yakiwamo ya upatikanaji
ardhi, ulinzi na uwekezaji.
Profesa alisema serikali hizo zinashirikiana
kwa ukaribu kuhakikiasha mradi huo unakamilika kwa wakati na kuanza kufanya
kazi mwaka 2020.
"Mradi upo na kasi ya utekelezaji ipo
lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 mradi unakamilika na sasa ni wakati wa
kila mtu kuwa tayari kwa ajili ya mradi huo," aliongeza Muhongo.
Waziri Muloni alisema alifurahi kuona jinsi
wananchi wa nchi hizo walivyo na shauku ya kuupokea mradi huo.
"Jana (juzi) nilitembelea maeneo
mbalimbali ya Tanga ikiwamo bandari sehemu ambayo bomba la mafuta litapita na niliona
ni jinsi wananchi wanavyoufurahia mradi huu, hivyo ni wakati sasa wa kufanya
kazi na wananchi, wajiandae," alisema Muloni.
0 comments:
Post a Comment