Sharifa Marira, Dodoma
Job Ndugai |
RIPOTI ya utekelezaji wa ufungaji vifaa
vya mashine za utambuzi wa vidole katika Jeshi la Polisi ulifanywa na kampuni
ya Lugumi imetua mezani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Ripoti hiyo ambayo iliagizwa na Bunge
ndani ya miezi mitatu tangu Juni 30 iliwasilishwa jana kwenye Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali (PAC) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projestus Rwegasira.
Mwenyekiti wa PAC, Naghenjwa Kaboyoka aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa Katibu Mkuu huyo alifika PAC jana na kutoa taarifa
kuhusu kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Bunge.
Alisema kwa kuwa taarifa hiyo imemfikia
Spika Ndugai ndiye atakayeiwasilisha kwenye Kamati hiyo kutokana na kwamba Bunge
ndilo liliagiza awali.
Alibainisha kuwa baada ya Katibu Mkuu wa
Wizara kutoa taarifa kwa Kamati juu ya kuwasilishwa kwa taarifa ya utekelezaji
wa maagizo ya Bunge, PAC haijaijadili taarifa hiyo.
Juni 30 wakati wa kuahirishwa Bunge la Bajeti,
Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, alisema Bunge liliiagiza Serikali
kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi na pia PAC ifuatilie na kutoa taarifa kwenye
taarifa yake ya mwaka.
Alisema Kamati ilibaini kuwa mradi huo
unafanya kazi katika vituo 14 pekee kati ya 108 jambo ambalo lilikuwa linakwenda
kinyume na mkataba.
Dk Tulia alisema kutokana na changamoto
hiyo, PAC ilimtaarifu Spika ambaye aliwaruhusu kuunda kamati ndogo ambayo nayo
ilifanya ukaguzi na kubaini upungufu.
Naibu Spika alisema baada ya kamati hiyo
kupitia ilikubaliana kukabidhi taarifa hiyo kwa Spika ambaye naye aliona kuwa
inastahili kuwasilishwa.
Alisema kwa mujibu wa kanuni ya 117(17)
Spika ataweka utaratibu wa kujadili taarifa ya Kamati na endapo kamati yoyote
katika utekelezaji wa majukumu yake, itaona kuna mambo ya utekelezaji, iyatoa
taarifa maalumu kwa Waziri husika ili achukue hatua stahiki.
Katika sakata ilo, Lugumi Enterprises
inadaiwa kupewa zabuni na Polisi kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama
za vidole katika vituo 108 nchi nzima kwa gharama ya Sh bilioni 37.
0 comments:
Post a Comment