Joyce Kasiki, Dodoma
MBUNGE wa Kongwa,
Job Ndugai (CCM), amewatolea uvuvi watumishi wa Halmsahuri ya Wilaya ya Kongwa
wanaomchukia akisema haoni sababu kwa watumishi hao kumchukia.
Akizungumza
kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa halmshauri hiyo, Ndugai alisema licha ya
yeye kuwa mstaarabu miongoni mwa wabunge wa sasa, anashangaa chuki dhidi yake akihoji
inatoka wapi.
Kabla hicho
kilichofanyika mwishoni mwa wiki Ndugai ambaye pia ni Spika wa Bunge, alikuwa
hajawahi kuhudhuria vikao vya baraza hilo tangu aliporejea kutoka nchini India
kwa matibabu.
"Namshukuru
Mungu kwa sababu halikuwa tarajio langu kama ningeweza kuiona siku hii miezi
machache iliyopita, nimepita katika mazingira magumu, nilikuwa na hali
ngumu kiafya…; wapo waliofurahi, wengine walisikitika, lakini nimepata nafasi
ya kujua binadamu wakoje.
Kwa waliofurahi
nilijiuliza maswali, hivi kumbe mimi kumbe ni mzigo, lakini nikajiuliza
kama ni mzigo ni kwa kipi, sioni
sababu ya kunichukia, lakini ukweli utabakia pale pale kwamba tuishi vizuri na
tusaidiane," alisema.
Aliwataka
madiwani na watumishi wa halamshauri hiyo kushirikiana katika utendaji kazi na
kutoa ushirikiano kwa mkurugenzi wa halamshauri hiyo na Mkuu wa Wilaya ya
Kongwa ambao ni watumishi wapya ili Kongwa iendelee kustawi kimaendeleo.
"Naomba
tusiwaingize hawa wakuu wetu katika zile mila na destur zetu za
uongo,kudanganya,mtu unataka DC (Mkuu wa Wilaya), apigane vita yako kwa
sababu tu wewe una ajenda zako,tuachane na hayo haisaidii hakmashauri,tuangalie
suala la maendeleo zaidi," alisema
Amewataka viongozi
na watumishi wote kufanya kazi kwa uadilifu ili kuepuka adha ya kutumbuliwa kwa
kutofuata maadili ya kazi zao.
"Usitegemee
kwa sababu wewe ni Diwani ukaenda kujenga daraja, zahanati ukaweka mrija wako
pale ili uishi, hizo enzi zimepita, awamu hii ikiletwa hela fulani
kufanya kazi ya Serikali hiyo ni ya Serikali, enzi zile za
kujineemesha mwenyewe kwa ujanja ujanja zimepita, maana wananchi walchagua
mabadiliko na haya ndio mabadiliko yenyewe," alionya Ndugai
Alisema anaamini
Serikali inaendelea kujenga miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kusogea huduma
karibu na wananchi hususan miundombinu ya umeme.
0 comments:
Post a Comment