Mwandishi Wetu
MTABIRI maarufu nchini, Hassan Hussein
ametabiri mambo 20 yatakayojiri mwaka huu 2017, ikiwemo viongozi walioikimbia
CCM na kujiunga na upinzani kurejea kwenye chama hicho tawala.
Ingawa Hussein hakuwataja viongozi hao,
waliotikisa walipotangaza kung’atuka CCM ni waliokuwa mawaziri wakuu kwa
nyakati tofauti; Edward Lowassa na Frederick Sumaye.
Lowassa aliihama CCM baada ya kukatwa
kwenye mchakato wa kuwania urais kupitia chama hicho mwaka juzi na hivyo
kujiunga na Chadema ambako alipitishwa kuwania urais akiungwa mkono na vyama
vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Sumaye aliungana na Lowassa baadaye na
akachaguliwa kuwa meneja wa kampeni za mgombea huyo aliyeshindana vikali na aliyekuwa
mgombea wa CCM kwenye uchaguzi huo, John Magufuli.
Mbali na utabiri huo, Hussein alisema hali
ya uchumi itaimarika zaidi mwaka huu na hali ngumu ya maisha iliyokuwepo mwaka
2016 itatoweka.
Aidha, amemtabiria Rais John Magufuli
kupata nishani ya juu ya dunia kutoka kwa Rais wa moja ya mataifa makubwa
duniani kutokana na uongozi wake, huku akitabiri viongozi waliokimbia chama
tawala CCM na kwenda upinzani, watarejea.
Maalim Hussein ambaye ni mtoto wa
aliyekuwa mtabiri maarufu, marehemu Sheikh Yahya Hussein, katika utabiri wake
wa mwaka 2017 ametabiri mambo 20 kutokea nchini likiwamo la viongozi wengi wa
kisiasa na kidini kukumbwa na kashfa ya ngono na wengine kujiuzulu nyadhifa zao
kutokana na kashfa za kiuongozi.
Alisema mwaka huu umeanza siku ya Jumapili
na kwa mujibu wa utabiri siku hiyo inashabihishwa na sayari ya jua ambapo
kinyota yake ni Simba, ambayo asili yake ni moto.
Pia huonesha kuwa nia ya ufalme ,
utawala na uongozi wa dini na kisiasa."Sayari hii inahusika na kiburi,
kutumia nguvu, ufahari, kuona haya, mambo ya kisiasa, udereva kwa maana vyombo
vya moto na mambo ya ufundi magari.
"Mwaka unapoanza Jumapili unaonesha
kuwa utakuwa baridi, yaani hautakuwa na rabsha nyingi lakini hautaki uharaka wa mambo.Kikubwa kuliko vyote
ni kwamba mambo huenda pole pole na yanahitaji subira kwa wale wanotaka
mafanikio,"alisema.
Maalim Husseina aliongeza mwaka
unapoanza Jumapili au kutumia tangaza
utabiri huo jijini Dar es Salaam jana, Maalim Hussein ambaye ni mtoto wa
aliyekuwa mtabiri maarufu Afrika Mashariki mara nyingi wa kijicho, watu na hasa
wanasiasa, viongozi wa dini na wa familia kuoneana husda na watu kada hiyo
hujikuta wakikumbwa na vifo vya kawaida au vya kuuawa na kuuana.
Alieleza kutokana na hali hiyo mwaka
2017 utakuwa mgumu wa mambo, mabishano ya kisiasa, kijamii na mataifa
mbalimbali kuhasiamiana,
Alisema kutokana na mwaka huu ulivyo
kinyota mambo mengine ambayo anatabiri kutokea ni kuzama kwa meli kwenye moja
ya habari kuu za dunia na ndege moja ya taifa kubwa duniani kuanguka na hivyo
kusababisha vifo vya watu kadhaa.
Pia ametabiri kutokea mvutano wa
kimtazamo na sera utakaosababisha mabadiliko makubwa ya uongozi wa serikali
duniani na Tanzania ikiwamo ambapo baadhi ya wanasiasa watapotea kabisa katika
uliongo wa siasa.
Maalim Hassan alitabiri viongozi wa dini
kutoa matamshi ya kutatanisha ambayo yanaweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa
amani na utulivu.Pia ametabiri muanguko wa vyama vya tawala katika nchi
mbalimbali duniani.
Pia ametabiri kutokea ajali nyingi
ambazo zitawakuta wanasiasa, watawala na viongozi wa dini katika mwaka 2017 na
kufafanua wimbo la vifo lililoikumbuka tasnia ya habari mwaka 2016 duniani
kuendelea kwenye mwaka huu wa 2017.
Maalim Hassan alitabiri vifo vya ghafla
vya kawaida vya wasanii maarufu duniani na Tanzania ikiwamo na vinaweza
vikatokana na fumanizi, kuuliwa na kuana wenyewe.
Pia ametabiri kuwa mwaka 2017 utakuwa ni
mwaka wa mabadiliko makubwa katika tasnia tofauti za kisiasa, kimichezo,kidini
na kiburudani kwa maana ya kwamba wale waliokuwa wakiongozwa au kunawiri katika
sekta hizo kushindwa katika chaguzi zao, kuondolewa kwa nguvu au kukataliwa na
watu.
Katika utabiri wake Maalim Hassan
alitabiri kifo cha chama kimoja maarufu cha siasa hapa nchini.Hata hivyo
hakutaja ni chama gani licha ya kufafanua kuwa CUF iko kwenye migogoro lakini
si lazima kiwe chama hicho.
"Maana wapo wanaweza kudhani
amekitabiria lakini ukweli kwenye utabiri huwa halengi mtu au kutaja jina ila
watanzania wasubiri kuona matokeo ya utabiri wake na kueleza katika miaka sita
ya kuifanya kazi hiyo kila ambalo anatabiri basi linatokea kwa asilimia zaidi
ya 96,"alisema.
Alisema mwaka huu utabiri wake unaonesha
CCM kushika hatamu zaidi itakayoleta maendeleo makubwa kwa chama hicho na nchi
ya Tanzania kwa ujumla.
Maalim Hassan alipotakiwa kuwataja
viongozi gani waliondoka CCM na kwenda upinzani na sasa anwatabiria kurudi ni
akina nani hakuwa tayari kutaja majina yao.
Alisema kwenye utabiri wake hataji mtu
ingawa anajua wapo viongozi kama Edward Lowasa(Waziri Mkuu wa zamani), Kingunge
Ngombari-Mwiru , Hamisi Mgeja, Laurance Masha na wengine wengi waliondoka CCM
na kwenda upinzani.
"Najua wapo watakaoanza kuwataja
viongozi hao, lakini niseme tu katika kutabiri huwa sitaji mtu wala kumlenga
mtu, hivyo tunatakiwa kusubiri kuona haya ambayo nimebari na kila ninapotabiri
huwa nafuatilia ili kujua yapi yametokea na yapi hayakutokea,"alifafanua
Maalim Hassan.
Kuhusu utabiri wake kuonesha mafanikio
makubwa kwa Serikali ya Rais John Magufuli alisema, Rais ni kiongozi wa nchi
hivyo utabiri ukionesha mema au mabaya lazima ayaseme kwa kutaja jina lake
maana anawahusu Watanzania wote.
"Katika utabiri nimezungumzia
mafaniko ya Rais Magufuli kwa kutaja jina lake na kwa nafasi yake lazima
ninapotoa utabiri unamhusu yeye nitaje jina lake ingawa kwa wengine siwezi
kutaja majina yao bali naeleze kile ambacho kinaonekana katika
utabiri,"alisema Maalim Hassan.
Alishauri kuwa vifo na maafa ambavyo
ametabiri vinaweza visitokee iwapo watu wataacha rabsha na uharaka wa kufanya
mambo kama nyota ya mwaka 2017 inavyosema.Pia watu waache chuki binafsi, choyo,
kuchonganisha na ngono isiyokubalika kisheria katika masuala ya siasa, jamii,
utawala na mamlaka.
Alipoulizwa vipi kuhusu waandishi wa
habari ambao waliandika habari zinahusu Mchungaji Lusekelo kudai waandishi
walimuandika watakufa, Maalim Hassan alisema hakuna mwandishi atafariki dunia
kwasababu ya kumuandikia mchungaji huyo ila ni matokeo ya kuelekea kwenye
anguko lake.
0 comments:
Post a Comment