Haji Kameta
Mwalimu Julius Nyerere |
WATANZANIA wametakiwa kuishi kwa kuenzi
falsafa za baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili kuifanya jamii kuwa mahala
salama pa kuishi.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Kitengo
cha Falsafa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk. Adolf Mihanjo ambaye
alifafanua kuwa watu wanatakiwa kufanya tafakuri ya kina kuhusu dini kuepuka
migogoro.
Alisema hayo katika mkutano wa amani
ulioandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu
wa Iran na kufanyika semina ya siku moja.
"Inatakiwa vijana wafundishwe
kufikiri kwa kina ili kupata ufumbuzi wa fikra na katika hilo tutashirikiana na
wenzetu wa Iran kwani wao wanauwezo mkubwa katika ukombozi wa
fikra,"alisema.
Mwalimu wa Falsafa na dini, Evarist
Magoti alisema yeye ni mwakilishi wa dini za jadi na amani. Alisema kuwa
waumini wa dini za sasa wanatakiwa kujifunza kupitia dini za jadi kwa maana hizo
zina historia kutokana na ukweli kuwa ndizo zilizopokea Ukristo na Uislamu.
"Tunatakiwa kuziangalia dini za
jadi kwa sababu zina uzoefu wa kuishi na dini zote na kutunza amani kwa muda
wote, hivyo ili tupate amani tunatakiwa kulinda tamaduni zetu," alisema.
0 comments:
Post a Comment