Grace Gurisha
Mahakamani |
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mhariri wa Gazeti
la Mawio, Simon Mkina, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi leo wanatarajia
kusomewa maelezo ya awali, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Mbali na Lissu na Mkina, washitakiwa wengine ni Jabir
Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.
Washtakiwa hao watasomewa maelezo hayo mbele ya Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Thomas Simba ambaye ndiye anayesikiliza kesi hiyo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
Jana washtakiwa hao walitakiwa kusomewa maelezo hayo,
lakini hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo kutokana na kwamba alikuwa na kesi
nyingine za kusikiliza..
Alisema kesi hiyo itasikilizwa mapema kwa sababu anakesi
zingine na kusikiliza.
Washtakiwa hao wanatetewa na Wakili Peter Kibatala. Awali,
hakimu huyo alishangaa upande wa Jamhuri kushindwa kumkamata Lissu licha ya
kwamba yeye alitoa hati ya kukamatwa kwa Mbunge huyo.
Hata hivyo, alimueleza Lissu kuwa aachane na mambo
anayofanya kwa sababu yeye ni kioo cha jamii, kwa hiyo hastahili kufanya
anayoyafanya na pia yeye ni mwanasheria na ajua sheria.
Ilidaiwa Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es
Salaam, washtakiwa watatu, Jabir, Mkina na Lissu, kwa pamoja waliandika na
kuchapisha taarifa? za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko
yaja Zanzibar’.
Wakati huohuo, Mahakama hiyo imeahirisha kesi nyingine ya
uchohezi ‘Dikteta uchwara’ inayomkabili Lissu kwa sababu upande wa Jamhuri
hawakuwa na mashahidi hadi Februari 14 mwaka huu kwa kusikilizwa.
0 comments:
Post a Comment