Leonce Zimbandu
Freeman Mbowe |
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema
atafunguka na kuzungumzia mambo yote yanayohusu deni linaloelezwa kuwa inadaiwa
hoteli yake ya Aishi Machame atakapofika jimboni kwake Hai.
Mbowe ametoa kauli hiyo baada ya gazeti hili
kumtaka azungumzie tuhuma zinazomkabili, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani
Kilimanjaro, Gellasius Byakanwa kudai amekwepa kulipa kodi ya huduma ya
biashara kwa miaka mitano.
Alisema kwa kipindi hiki hawezi
kuzungumzia sakata hilo hadi atakapowasili katika jimbo lake la Hai ili kujua
ukweli wa tuhuma hizo ambazo zimetangazwa na Mkuu wa Wilaya.
“Siwezi kuzungumza chochote, kwani
sifahamu kinachoendelea. Lakini nikifika jimboni nitafunguka na kubainisha
ukweli wa tuhuma hizo,” alisema.
Jana gazeti hili ilichapisha habari kuwa
baada ya sakata la Club Billicanas kuamiriwa kuhama katika jengo la Shirika la
nyumba la Taifa (NHC) mwaka jana kutokana na kudaiwa deni la sh.bilioni 1.3 la
pango.
Katika sakata hilo jipya la Hoteli ya
Aishi Machame Mkuu wa wilaya Byakanwa alidai kuwa Hoteli hiyo iliandikiwa barua
Januari 21, mwaka jana na kutakiwa kulipa kodi lakini barua hiyo haikujibiwa.
Mbali na barua hiyo kutojibiwa Byakanwa
alidai kuwa Hoteli hiyo haijapeleka taarifa ya mauzo ya kila mwaka katika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa miaka mitano kwani taarifa hiyo ingetumika
kukadiria kodi.
Kutokana na madai hayo, Byakanwa aliamua
kutoa siku 14 kwa Uongozi waHoteli hiyo kulipa kodi hiyo ya huduma ya biashara
inayofikia sh. milioni 13.5, vinginevyo huduma hiyo itasitishwa.
Katika hatua nyingine Byakanwa
amesitisha shughuli za kilimo katika shamba linalimilikiwa na Mbowe kwa madai
kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji yam to Weruweru.
Hivyo aliagiza Baraza la Taifa la
Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika
eneo hilo uliofanywa na Mbunge wa Hai ili hatua zichukuliwe.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Hai Byakanwa
aliwataka maafisa Maliasili wa Wilaya kufanya tathmini ya miti iliyokatwa bila
kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14 ili hatuya zifanyike.
“Huyu ni kiongozi wa kitaifa tena kioo
cha jamii anapaswa kuwa mfano kwa wananchi anaowangoza, sfanyi hilo kwa
kumwonea mtu hali nazingatia sheria,” alisema.
0 comments:
Post a Comment