Grace Gurisha
UPANDE
wa Serikali katika kesi ya Yusuf Yusuf ‘Mpemba’ (34) umeiambia Mahakama kuwa upelelezi
umekamilika na jalada la kesi liko kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Kanda ya Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
Awali,
Jamhuri uliiambia Mahakama hiyo juzi kuwa jalada hilo liko kwa Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro analifanyia kazi ili
liende ngazi zingine kwa hatua zaidi.
Mkuu
huyo akishamaliza kulifanyia kazi atalipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP), Biswalo Mganga kwa hatua zaidi za kulitolea uamuzi atakaoona unafaa
katika kesi hiyo ili iendelee.
Awali, Wakili
wa Serikali, Patrick Mwita alimwambia Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba,
kuwa mara ya mwisho Mahakama iliwataka watoe maelezo ya lilikofikia jalada
katika upelelezi.
“Licha
ya kwamba upelelezi umekamilika, lakini bado jalada liko kwa Kamanda Siro
analifanyia kazi kabla ya kulipeleka kwa DPP kwa hatua nyingine,” alidai Mwita.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 23 itakapotajwa.
Mbali na
Mpemba ambaye ni mkazi wa Tegeta, washitakiwa wengine ni Charles Mrutu (37) wa
Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) wa
Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46).
Washitakiwa
hao wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa ujangili na biashara ya meno ya tembo
yenye thamani ya Sh milioni 785.6.
Ilidaiwa
kuwa katika tarehe zisizofahamika kati ya Januari 2014 na Oktoba, mwaka jana
wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walikusanya na kuuza vipande 50
vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 mali
ya Serikali bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Aliendelea
kudai kuwa katika mashitaka ya pili, Oktoba 26 mwaka jana washitakiwa wakiwa
Mbagala Zakhem, Temeke walikutwa na vipande 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 na
thamani ya dola 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.
Ilidaiwa
kuwa katika mashitaka ya tatu, Oktoba 27 mwaka jana washitakiwa wakiwa Tabata
Kisukuru, walikutwa na vipande vinne vyenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya
dola 15,000 sawa na Sh milioni 32.7.
Pia
Oktoba 29 mwaka jana walikutwa na viapande 36 vya thamani ya Sh milioni 294.6.
0 comments:
Post a Comment