Hussein Ndubikile
Profesa Joyce Ndalichako |
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako amsema shule za sekondari zipatazo 1,629 zitagawiwa
vifaa vya maabara mwezi huo.
Alisema vifaa hivyo vitagawiwa kwa shule
zote ambazo zimekamilisha ujenzi wa maabara, huku akisisitiza shule
zinazoendelea na ujenzi huo kukamilisha haraka.
Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo
katika hafla ya kuzipongeza halmshauri kumi zilizofanya vizuri katika
utekelezaji wa mpango wa lipa kulingana na matokeo.
Katika hatua nyingine alizitaka halmashauri
zote nchini kuhakikisha zinasimamia vyema upangaji na urekebishaji wa ikama za
walimu kwa kuwatawanywa sehemu husika kwa kuzingatia mahitaji ili kuleta tija
katika sekta ya elimu.
Alisema sababu kubwa inayosababisha
halmashauri nyingi kutofanya vizuri katika sekta hiyo ni upangaji wa walimu
usiozingatia mahitaji ya maeneo hali inayozorotesha ufaulu wa wanafunzi.
“Serikali bado haijafurahishwa na
halmashauri jinsi zinavyopanga walimu wilayani ndio maana zinashindwa kufanya
vizuri kwenye matokeo,” alisema.
Alisema halmashauri zilizoshinda fedha
taslimu zilizingatia ufuatiliaji wa suala hilo, uandaaji wa takwimu za shule
kwa usahihi pamoja na matumizi sahihi ya ruzuku za uendeshaji wa shule.
Alizitaja halmshauri hizo kuwa ni Wilaya
ya Kaliua, Muleba, Geita, Bunda,Rorya, Nzega, Ngara, Itilima, Kongwa na Chato.
Alizigiagiza halmashauri hizo kuzitumia
fedha ilizozipata katika urekebishaji wa ikama ya walimu, ujenzi wa madarasa,
vyoo na ukamilishaji wa maabara.
0 comments:
Post a Comment