Hussein Ndubikile
Rais John Magufuli |
RAIS John Magufuli ameanza kuhudhuria Mkutano
wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea mjini Addis Ababa,
Ethiopia.
Taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya
habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya
Rais, Gerson Msigwa ilieleza kuwa jana asubuhi Rais Magufuli alihudhuria mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wa umoja
huo, Idriss Deby Itno na kwamba wakuu wa nchi za umoja huo watakutana na Katibu
Mkuu Mpya wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres.
Malengo ya mkutano huo ni kubadilishana
mawazo juu ya namna ya kuboresha uhusiano kati ya umoja huo na UN hususan
katika kuimarisha masuala ya usalama.
Msigwa alisema kuwa mkutano huo
utafuatiwa na mkutano maalumu wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika utakaongozwa
na mwenyekiti wake.
Alisisitiza kuwa rais Magufuli alikula
chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika (AUC),
Dk. Nkosazana Zuma lengo likiwa kutangaza rasmi jina la kituo kipya cha usalama
na amani kilichopewa jina la Mwalimu Julius Nyerere kutokana na kutambua
mchango wake katika kupigania amani na usalama wa Afrika.
Pia, alisema kituo hicho kipo ndani ya
majengo ya Makao Makuu ya AU mjini humo,
huku akiongeza kuwa rais Magufuli alitoa hotuba fupi baada ya kukitangaza.
0 comments:
Post a Comment