Laonce Zimbandu
Dk Yahya Msulwa |
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi
Tanzania (Tucta) limesema litapigania sheria ya kulipwa kima cha chini cha mshahara
kinachomwezesha mfanyakazi kumudu mahitaji.
Sheria ya kima cha chini haizingatii
kumwezesha mfanyakazi wa ngazi ya chini kumudu mahitaji muhimu ya maisha,
ikiwamo chakula, malazi, matibabu na elimu kwa watoto.
Hivyo, kima cha chini kinachomwezesha
mfanyakazi kumudu mahitaji ni Sh 750,000 au zaidi badala ya Sh 315,000 kiilichotangazwa mwaka
2006.
Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahya Msulwa,
alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu
vipaumbele vya utendaji wa Tucta mwaka huu.
Alisema tangu mwaka 2006 Tucta ilifanya
utafiti kujua kima cha chini cha mshahara kinachomwezesha mfanyakazi kumudu
maisha kuwa ni Sh 315,000 kwa mwezi na Serikali ikaombwa isikate kodi, lakini
hilo halikufanyika.
“Kuanzia mwaka 2014 mshahara wa Sh 750,000 ulitakiwa usikatwe kodi ili
kupunguza uwiano wa makato ya kodi ya mishahara kwa ngazi zingine, hivyo kodi
isizidi kiwango cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni asilimia 18,” alisema.
Dk Msulwa aliiomba Serikali kupunguza
utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii ili kupunguza gharama za uendeshaji na
kuondoa tofauti ya mafao kati ya mifuko hiyo kwa wanachama.
Alisema Tucta inaomba mifuko hiyo
ipungue na kubaki miwili yaani mfuko wa watumishi wa umma na mfuko wa hifadhi
ya jamii kwa watumishi wa sekta binafsi.
Taaluma
Dk Msulwa alisema Serikali inapaswa
kuangalia namna ya kulinda wataalamu wa elimu ya kati, ikiwamo vyuo vya Stashahada
ya Ufundi ambavyo vimegeuzwa kuwa vyuo vikuu, hivyo uzalishaji wa wataalamu wa
ngazi ya kati kupungua.
Alisema ni ajabu kuzungumzia wataalamu
wenye Shahada na Shahada za Juu huku
wakisahau kuwa kila mhandisi anatakiwa kuwa na wataalamu wanne wenye Stashahada
huku mwenye Stashahada akitakiwa kuwa na wataalamu kati ya sita na 10
wenye cheti.
Alishauri siasa isifunike utaalamu kwa
vile maendeleo hayawezi kupatikana bila kuhusisha wataalamu katika maeneo mbalimbali,
ikiwamo utungaji wa sera na utoaji uamuzi.
Adhabu
Tucta imesisitiza kuwa utoaji adhabu kwa
watumishi wa umma kwa makosa mbalimbali yanapaswa kuzingatia sheria
zinazotawala mambo ya kazi na ajira, ikiwamo kushirikisha mamlaka zao.
Watumishi wanapaswa kupewa fursa ya
kujieleza kwenye Bodi au Tume iundwe kwa ajili ya kuchunguza ukweli wa kosa ili
hatua ichukuliwe.
“Itakuwa si busara kwa kila kiongozi
hata kama hana mamlaka ya kutoa adhabu akaagiza adhabu bila kufuata taratibu,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment