Peter Akaro
ZAIDI
ya Sh 13.07 trioni zimepita katika mitandao ya simu katika kipindi cha miezi
miwili iliyopita, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra), imesema.
Kaimu
Meneja wa Mawasiliano, Semu Mwakyanjara alisema jana kuwa kiasi hicho cha fedha
kilipita kwenye mitandao hiyo kati ya miezi ya Novemba na Desemba.
“Mwishoni
mwaka jana kwa mwezi Novemba na Desemba kwa wastani fedha zilizopita katika
mitandao ya kampuni za simu Sh. trilioni 13.07,” alisema Mwakyanjara na
kuongeza;
“Kwa
mwezi Novemba ilikuwa ni Sh. trilioni 6.47 na Desemba Sh. trilioni 6.60.”
Katika
hatua nyingine, Semu alitoa tahadhari kwa wananchi wanaotumia huduma za
kuhamisha fedha kupitia simu za mkononi kwamba kuna matapeli wanaoghushi taratibu
za huduma hiyo.
Akizungumza
jana Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mahusiano kwa Umma, Semu Mwakyanjara alisema
kumekuwa na ongezeko la matapeli wanaotuma ujumbe mfupi unaokaribia kufanana na
ule wa watoa huduma.
“Upokeapo
taarifa kuwa umetumiwa fedha kwa makosa na kufuatiwa na ujumbe mfupi unaofanana
na ujumbe wa watoa huduma, kisha kutakiwa kurudisha fedha hizo, unachotakiwa ni
kujiridhisha kwanza.
“Omba
taarifa fupi ya akauti yako kwa watoa huduma ili uhakiki miamala yako na salio
lako, ikibidi wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja,” alisema.
Mwakyanjara
aliwataka wananchi kutotoa taarifa zozote kuhusu namba zao za simu au taarifa
binafsi kwa mtu yeyote ambaye atawapigia simu.
“Ukipoteza
simu au laini toa taarifa kwa watoa huduma na polisi na ukifanyiwa uhalifu na
simu yako imetumika, toa taarifa ili wahalifu wasakwe,” alisema.
0 comments:
Post a Comment