Leonce Zimbandu
Askofu Valentino Mokiwa |
MSEMAJI wa Askofu Valentino Mokiwa wa
Kanisa la Anglican Dayosisi ya Dar es Salaam, Yohana Sanga amesema kanisa hilo litaendelea
kuongozwa kwa kuzingatia vikao halali vitatu, kikiwamo kikao cha nyumba ya maaskofu
ambacho ni chombo kinachotoa dira na mwelekeo wa kanisa.
Kikao kingine ni wajumbe wa sinodi
pamoja na Kikao cha Halmashauri ya Kudumu ya Kanisa, hivyo maamuzi
yatakayotolewa katika vikao hivyo ndiyo yatakayozingatia taratibu za kanisa.
Sanga aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na gazeti hili katika Kanisa la Mtakatifu Albano lililopo eneo la
Posta jijini Dar es Salaam jana.
Alisema Askofu Valentino Mokiwa
ataendelea kuwa Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam, licha ya taarifa kwamba
hatajihusisha tena na huduma.
Aliongeza kuwa Askofu Mokiwa hana mipaka
ya eneo la kuabudu kwa sababu makanisa ya Anglican jijini Dar es Salaam yapo
chini ya uangalizi wake.
“Leo (jana) sijawasiliana na Askofu huenda
amekwenda kuabudu kanisa jingine, lakini jimbo halina taarifa rasmi na kile
kilichotangazwa kwenye vyombo vya habari bali Mokiwa bado ni Askofu wa Jimbo la
Dar es Salaam,” alisema.
Alisema sakata hili limeanza muda mrefu,
kwani Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania, Askofu Jacob Chimeledya aliandika
waraka wa kumtaka Askofu Mokiwa ajiudhuru, baada ya kanuni kutozingatiwa uamuzi
huo ulishindikana.
Imedaiwa kuwa chanzo cha mgogoro huo ni
baada ya Askofu Valentino Mokiwa kuhamisha Mapadre kutoka kanisa moja kwenda
jingine, hivyo mmoja wa Mapadre hao aligoma kuhama.
Hali hiyo ilimlazimu Askofu Mokiwa
kumvua upadre, hata hivyo aliendelea kukaidi hatua hizo zilizochukuliwa na
Askofu wa jimbo na kupelekea kiongozi huo kwenda kutoa malalamiko kwa Askofu
Mkuu wa Kanisa hilo mjini Dodoma.
Haijafahamika kama vikao halali vya
maamuzi vya kanisa hilo vimekaa na kujadili changamoto hiyo kabla ya kutoa
maamuzi au la, hivyo kila muumini wa kanisa hilo bado haelewi hatima ya mvutano
huo ndani ya kanisa.
0 comments:
Post a Comment