Aidan Mhando, Mwanza
SIKU chache baada ya wavuvi 2,000 wa
Ziwa Victoria kutangaza mgomo kwa siku zisizojulikana kwa madai kuwa Serikali
inawakandamiza kutokana na sheria mbovu ya uvuvi, Serikali imesema mgomo huo ni
faida, kwani itatoa nafasi ya kukua kwa rasilimali zilizopo kwenye Ziwa hilo.
Kauli hiyo inakuja ikiwa tayari Jeshi la
Polisi mkoani hapa kwa kushirikina na Hifadhi ya Usimamizi wa Rasilimali za
Ziwa Victoria, kukamata wavuvi haramu 14 na zana haramu za uvuvi ikiwamo nyavu
1,660.
Akizungumza na gazeti hili jana, Ofisa
Mfawidhi wa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi Kanda ya Mwanza, Lameck Mongo
alisema mgomo huo kwao ni faida, kwani utasaidia kuongezeka samaki ambao
wamekuwa wakivuliwa kinyume na sheria.
“Serikali itahakikisha hatua stahiki
zinachukuliwa kwa watakaoshiriki uvuvi kinyume na sheria za uvuvi zinavyotaka. Watu
wanapaswa kutii sheria na kuacha kutafuta sababu zisizo na msingi. Hatuwezi kuacha
watu watumie nyavu zisizoruhusiwa kuvua samaki,” alisema Mongo.
Mongo alisema watu waliotangaza mgomo
huo ni kikundi cha wachache, kwani bado shughuli za uvuvi zinaendelea Ziwa
Victoria kama kawaida na waendelee na mgomo huo tu kama wanataka.
Alisema sheria ya uvuvi ya mwaka 2003
kifungu cha 22, inatoa maelekezo ya uvuvi ikiwamo kuzuia kuvua kwa zana haramu
na kanuni za sheria hiyo za mwaka 2005 kifungu cha 52, H, K zinakataza kuunganisha
nyavu haramu.
Hivi Karibuni, Msemaji wa Chama cha
Wavuvi Kanda ya Ziwa (TAFU), Sijaona James alisema wanataka na mazungumzo ili kupata
majibu ya pamoja ikiwamo Serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya uvuvi.
Serikali imekuwa ikiendesha operesheni dhidib
ya uvuvi haramu, ikiwamo katika Ziwa Victoria.
0 comments:
Post a Comment