Salha Mohamed
JOPO la madaktari wa Taasi ya Tiba ya
Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MoI), limeridhia kijana Baraka Mashauri (35)
mwenye urefu wa futi 7 anayesumbuliwa na nyonga akatibiwe nje ya nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Ustawi
wa Jamii cha Moi, Jumaa Almas alisema madaktari hao waliokuwa wanafuatilia
matibabu ya Mashauri walifikia hatua hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto.
“Tumeamua kumpeleka nje ya nchi baada ya
kubaini kuwa gharama za matibabu yake kwa hapa nchini ni kubwa,” alisema na
kuongeza kuwa alihitajika kuwekewa pandikizi (implant) kinachotakiwa kuagizwa
nje ya nchi.
Almas alisema pamoja na kupunguza
gharama za matibabu zinazogharamiwa na Serikali, kutibiwa nje kutawezesha
kupatikana matibabu ya uhakika na uhakika wa pandikizi kuliko hapa nchini
ambapo zingeagizwa tatu kutoka nje ya nchi ili kupata moja ya inayofaa.
“Ikumbukwe kwamba vifaa hivyo (pandikizi)
vinatengenezwa kwa `oda’ maalum hivyo gharama ni za juu ikilinganishwa na
kupelekwa nje ya nchi,”alisema.
Mashauri ni mgonjwa wa kwanza kupokelewa
MoI akiwa na urefu ambao haujawahi kudhihirika kwa mwingine kabla na baada ya
kufika hospitalini hapo mwishoni mwa Oktoba mwaka juzi, akitokea Majita B
mkoani Mara, ili kutibiwa nyonga kwenye mguu wa kushoto.
Kwa mujibu wa Almas, mgonjwa huyo
ameibua changamoto nyingi zinazotokana na urefu wake ikiwamo kushindwa kupata
kitanda miongoni mwa vinavyotumika kwa wagonjwa wa upasuaji vyenye urefu wa
futi sita.
0 comments:
Post a Comment