Mwandishi Wetu
Zitto Kabwe |
KIONGOZI wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe,
amesema iwapo Serikali itamudu kugawa tani milioni 1.5 za chakula zilizobaki
msimu uliopita katika maeneo yenye uhitaji mkubwa ili kupunguza kasi ya
ongezeko la bei za vyakula nchini, atajiuzulu ubunge.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini
amesema Serikali haina kiasi hicho cha chakula kwa maelezo kuwa mpaka Oktoba
mwaka jana kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu kwenye maghala yote ya Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).
Kauli ya Mbunge huyo imekuja siku moja
baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusema Serikali itachukua jukumu hilo,
kwamba katika msimu uliopita, kulikuwa na zaidi ya tani milioni tatu ila baada
ya wabunge kushinikiza Serikali kuruhusu kuuza vyakula nje, kiasi cha tani
milioni 1.5 ziliuzwa na hivyo kubaki tani milioni 1.5.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi
na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba, Serikali kupitia NFRA
katika mwaka wa fedha wa 2016/17 imepanga kununua tani 100,000 za chakula, hadi
Januari 8 mwaka huu, wakala huo ulishanunua tani 62,087 za mahindi.
Tizeba alisema hadi Januari 12, NFRA
ilikuwa na tani 88,152 za akiba ya chakula katika maghala yake.
Lakini jana kupitia akaunti yake ya
mtandao wa kijamii wa Facebook iliyothibitishwa na ofisa habari wa chama hicho,
Zitto alisema haiwezekani Serikali imudu kugawa kiasi hicho cha chakula wakati
NFRA kuna kiasi kidogo cha chakula.
“Tunashukuru wa hivi sasa ajenda ya
tishio la njaa inapata majibu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa kuibua
masuala muhimu kwa nchi yetu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment