Suleiman Msuya
John Shibuda |
MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa
nchini, John Shibuda, amesema atatolea ufafanuzi kuhusu hatima ya mvutano ulipo
kati ya vyama vya siasa na Serikali kuhusu mikutano ya hadhara ndani ya simu 21
zijazo.
Shibuda aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na vyombo vya habari, ikiwa ni takribani mwezi mmoja baada ya
kuchaguliwa na baraza hilo kuwa mwenyekiti, akichukua nafasi iliachwa na
aliyekuwa Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray.
Alisema tangu Serikali ya Awamu Tano iingie
madarakani hali ya kisiasa imekuwa na mvutano mkubwa na hali hiyo imekuwa
ikileta mivutano mikubwa.
Mwenyekiti huyo alisema ni jukumu la
baraza kukaa na kutafari kuhusu mvutano huo uliopo alioeleza kuwa hauna tija kwa
siasa za Tanzania.
Hata hivyo alieleza kuwa bado hakuna
budi kwa vyama kuangalia njia sahihi ya kuwasiliana na Serikali na kuachana na
tabia ya kutumia lugha zisizofaa ambazo zinasababisha kutofautina.
“Sisi kama Baraza tunahitaji vyama vya
siasa na wanasiasa kufanya siasa za maendeleo na si za kulumbana, kwani hazina
tija kwenye maslahi ya nchi,|” alisema.
Alivitaka vyama vya siasa kufikisha
madai yao kwenye baraza hilo ili liweze kuchukua hatua stahiki na kuachana na
utaratibu wa kila chama kuzungumza lake.
Shibuda alisema kauli za baadhi ya viongozi
wa vyama vya kisiasa zinaweza kuwa sababu ya Serikali kufanya maamuzi ambayo
yanalalamikiwa, hivyo kuwataka wasome alama za nyakati.
“Hakuna shaka kuwa mikutano ya kisiasa
miaka ya nyuma ilichangia kutetereka kwa Serikali iliyopita, hivyo wanapaswa
kutambua Serikali hii ni nyingine wanapaswa kusoma mazingira,” alisema.
Halikadhalika alisema pamoja na
changamoto zilizopo za kisiasa nchini, bado uhuru kwa vyama vya siasa
unahitajika ili kuhakikisha haki za kisiasa zinatekelezwa.
Shibuda alitumia mkutano huo kumpongeza
Rais John Magufuli kwa kile alichodai kuwa amefanikiwa kurejesha heshima ya
utumishi, kudhibiti mianya ya rushwa, ubadhirifu na wizi katika Serikali.
Aidha, alimpongeza Rais wa Zanzibar Dk.
Ali Mohamed Shein kwa kuiongoza nchi hiyo kwa kufuata misingi ya utawala bora
na kuwataka wananchi kumuunga mkono.
Alisema ni jukumu la wananchi kuwaunga
mkono ikiwa ni kwa kufanya kazi ambazo zitaongeza pato lao na kukuza uchumi wa
nchi na kuondoa matabaka ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu.
Katika mkutano huo ulikuwa na wajumbe wa
vyama vya siasa vicahche huku vyama vya upinzani vyenye wabunge vikiwa havina
wawakilishi.
0 comments:
Post a Comment