Mery Kitosio, Arusha
Patrobas Katambi |
MWENYEKITI wa Bavicha, Patrobas Katambi,
amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kuwachukulia hatua
askari ambao wanaenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Aliyasema hayo jana katika Ofisi za Makao
Makuu ya Chadema mkoani hapa alikokuwa akizungumzia masuala mbalimbali
yaliyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliokuwa unaendelea katika kata
ya Mateves na Ngarenanyuki.
Katambi alidai kuwa katika Kata ya Mateves
kumekuwa na uvunjifu wa demokrasia na utawala ambao umekuwa ukitumika katika
chaguzi hizo kwa baadhi ya walinzi wa CCM kuwateka na kuwashambulia kwa silaha
za jadi vijana wa Chadema ambao walikuwa kwenye maandalizi ya uchaguzi mdogo
uliofanyika jana.
"Kumekuwa na uvunjifu mkubwa sana
wa misingi ya demokrasia na Utawala wa Sheria kwa maana ya kutoheshimu sheria
za nchi zinazoongoza uchaguzi. Juzi katika kata ya Mateves walinzi wa CCM
waliwashambuliwa kwa silaha za jadi vijana wa Chadema mbele ya macho ya polisi,”
alisema.
Katambi aliwataja vijana watatu
walioshambuliwa kwa mapanga na rungu kuwa ni John Mwasele, Joseph Gabriel na
Baraka Juma.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha,
Charless Mkumbo alisema kuwa taarifa ya kukamatwa na kujeruhiwa kwa baadhi ya
vijana wa Chadema bado hajazipata ila atazifuatilia kujua chanzo chake.
0 comments:
Post a Comment