Peter Akaro
Ummy Nderiananga |
SHIRIKISHO
la Vyama vya Walemavu Tanzania (Shivyawata), limeipongeza Serikali kwa kusikia
kilio chao juu ya vifaa tiba, ila limebainisha kuwa suala la usafiri bado
changamoto kwao.
Mwaka
jana shirikisho hilo lililalamikia kauli ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu aliyebainisha kuwa kundi hilo linapaswa
kujigharamia vifaa tiba na matibabu.
Lakini
mwenyekiti wa Shivyawata, Ummy Nderiananga, alisema jana kuwa baadaye Waziri
Mwalimu alisikia kilio chao na akatoa agizo kwa hospitali kuendelea kuhudumia
watu wenye ulemavu.
“Pia
tuliomba bima ya afya kwa walemavu na Serikali ilishaanza mchakato wa kutupatia
na vitu vingine tulivyoomba ni kama mafuta ya albino na walishatupatia kwa hiyo
mambo yanaendekea vizuri,” alisema.
Nderiananga
alisema huduma hizo kwa kiasi kikubwa zimefika mikoani na wao kama viongozi hawajapata
shida au mamalalamiko kutoka huko.
Kuhusu
usafiri kwa walemavu ndani Maradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart),
Nderiananga alisema bado kuna changamoto.
Alitaja
changamoto hiyo kuwa ni kukosekana kwa nafasi ya kukaa watu wenye ulemavu
ingawa kwenye mabasi hayo kuna viti vilivotengwa kwa ajili ya makundi maalumu
kama wazee na wajawazito na walemavu.
Alisema
suala hilo wanajaribu kulishughulikia na pia kwenda mbali zaidi kwa kuangalia
kama walemavu wanaweza kusafiri kwa gharama nafuu au bure kabisa kwa sababu mradi
huo ni wa Serikali.
“Hili
linazungumzika na tumepanga kwenda huko kupata utatuzi wa hii changamoto,”
alisema Nderiananga.
0 comments:
Post a Comment