Magreth Magosso, Kigoma
MKAZI wa kijiji cha Mwamgongo mkoani
hapa Zubeda Said (33) anadaiwa kupigwa na mumewe hadi kuuawa baada ya kupoteza
Sh 200.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa jana, dada wa marehemu, Siwema Masoud alidai kuwa awali ndugu yake huyo
alimpigia simu kuwa Januari 19 usiku alipigwa na mumewe kwa kupotea Sh 200.
Alisema siku moja kabla alimpa mtoto wa
kaka yake mwenye umri wa miaka mitano Sh 200 akanunue maandazi, lakini mtoto
huyo aliporwa fedha hiyo na wenzake, akashindwa kurudi nyumbani kwa siku mbili,
akarudi siku ya ugomvi wa wawili hao na mumewe kukasirika.
Alidai kuwa mume huyo, Kunduwenda Kiza
(37) akimfokea mtoto huvyo mama mtu kuamua kumwomba radhi mumewe huyo lakini bila
mafanikio kwani katika hali ya kushangaza mumewe alimpiga mpaka kupoteza
fahamu.
Siwema asilimulia kuwa kesho yake saa
9.45 alfajiri hali ya Zubeda ilibadilika na kutokwa damu sehemu mbalimbali zilizo wazi mwilini
mwake, mumewe akamkimbiza kwenye zahanati ya kijiji hicho na Januari 20,
alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa ya Maweni.
Alisema
Januari 21, saa 12.45 Zubeda alipoteza maisha hali iliyowapa mashaka na
kufikisha taarifa Polisi kwa uchunguzi maiti
lakini walipokwenda na askari hospitalini wakaambiwa jalada halionekani.
Hata hivyo, mganga aliyetambuliwa kwa
jina la Dk Muganyizi alijitolea na kuufanyia uchunguzi mwili huo na baada ya
uchunguzi maiti alibaki mochari.
Lakini wakati ndugu wakijiandaa kwenda
kuchukua mwili walishangaa kukuta umeondolewa, na kwa msaada wa polisi
waliukamata ukisubiri kusafirishwa kinyemela.
Gazeti hili lilifika Maweni na kugundua kuwa
kabla ya kifo alilazwa wodi 2(b) ya wanawake huku jalada lenye taarifa zake likiwa
limetoweka huku uchunguzi wa Mganga ukibaini kuwa na majeraha ndani ya mwili yaliyosababisha
kuvuja damu kulikochangia kifo hicho.
JAMBO LEO ilibisha hodi kwa Kamanda wa
Polisi wa Mkoa, Ferdinand Mtui ambaye alikiri kupokea taarifa za kifo cha
kutatanisha cha Zubeda.
Kamanda Mtui alisisitiza kuwa mshukiwa
Kiza anashikiliwa na Polisi kwa upepelezi na ikibainika ametenda kosa
hilo, atafikishwa mahakamani.
0 comments:
Post a Comment