Grace Gurisha
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeutaka upande
wa Jamhuri kwenye kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili mfanyabiashara wa
Dar es Salaam, Hussein Ndama (44) kuharakisha upelelezi.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama
hiyo,Victoria Nongwa, baada ya Wakili wa Serikali Leonard Challo kumwambia kuwa
upelelezi bado haujakamilika.
Challo aliiambia Mahakama kuwa kesi ilikuja kutajwa,
upelelezi haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine ya kuangalia kama
utakuwa umekamilika.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi
hiyo hadi Januari 24, itakapotajwa. Mshitakiwa amepelekwa rumande kwa sababu
moja kati ya mashitaka yanayomkabili la kutakatisha fedha halina dhamana.
Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014 Dar es Salaam, alighushi
nyaraka za kibali cha kusafirisha madini na sampuli zao kuonesha kuwa
kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa
kusafirisha makasha manne ya dhahabu ya kilo 207 yenye thamani ya dola 8,280,000
kwenda Australia kwa kampuni ya Trade
TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
0 comments:
Post a Comment