Mery Kitosio, Arusha
Mrisho Gambo |
MKUU wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo,
anatarajia kupanda kizimbani kutoa ushahidi katika kesi ya kusambaza ujumbe wa
kuudhi kwa njia ya mtandao, inayomkabili mbunge wa Arusha Godbless Lema na mkewe
Neema.
Wengine wanaotarajia kutoa ushahidi
katika kesi hiyo ni mkuu wa upelelezi wa polisi mkoa wa Arusha, RCO George
Katabazi, mkuu wa upelelezi wa wilaya (OC CID), Damas Masawe na kampuni ya simu
ya Vodacom.
Lema (40) na Neema (33) wamepanda kizimbani
leo katika Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha na kusomewa maelezo ya awali katika
shauri la jinai namba 51 la mwaka 2016.
Mbunge huyo anashtakiwa kwa kosa la
kumtumia ujumbe kwa njia ya mtandao kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo
Akisoma maelezo hayo mbele ya hakimu, John
Baro wa mahakama hiyo, wakili wa Serikali Alice Mtenga alisema mshtakiwa Lema Agosti
20 mwaka 2016, alituma ujumbe kupitia simu yenye namba 0764170745 mali ya mkewe
Neema Lema kwenda namba 07667575757 mali ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mtenga alisema upelelzi wa kesi hiyo
umekamilika na wanatarajia kuleta mashahidi watano na vielelezo viwili ambavyo
ni simu ya mshtakiwa na karatasi yenye ujumbe wa mashtaka.
Wakili wa upande wa mshtakiwa
wakiongozwa na John Malya baada ya kusikiliza maelezo hayo, alisema kuwa hati
ya mashtaka imekosewa na kuitaka Mahakama iondoe shauri hilo mahakamani.
Hata hivyo, hakimu Baro aliahirisha kesi
hiyo hadi Februari 3, mwaka huu atakapotoa uamuzi au sikilizwaji wa kesi hiyo.
Wakati huo huo, kesi ya jinai namba 352
ya mwaka 2016 inayomkabili mbunge huyo imeunguruma leo mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo Lema anashtakiwa kwa
kosa la kuchochea maandamano ya kupinga udikteta maarufu kwa jina la Ukuta. Kesi
hiyo ilikuwa kwa hakimu mfawidhi Agustino Rwezile wa Mahakama ya Hakimu mkazi
Arusha. Kwa sasa kesi hiyo inasikilizwa na hakimu Bernad Nganga baada ya hakimu
Rwezile kuhama kikazi.
Mwanasheria wa Serikali, Alice Mtenga
aiiambia Mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, ambapo alisoma maelezo
ya awali kwa Mshitakiwa.
Hata hivyo, upande wa mstakiwa
ukiongozwa na wakili John Mallya walidai kuwa kesi hiyo inayomkabili mshtakiwa
ni yakikatiba kwani alilenga kutoa maoni yake kama mwananchi wa kawaida.
Alisema ibara ya 18 yakatiba ya jamhuri ya
muungano Tanganyika ya mwaka 77 inatoa haki kwa mshitakiwa ama raia mwingine
kutoa maoni yake.
Malya alisema kesi hiyo inapaswa
kusikilizwa na mahakama ya katiba chini ya majaji watatu, jambo ambalo hakimu
Nganga alisema atalitolea uamuzi mdogo Februari 8 mwaka huu.
Mbunge Lema alirudi magereza kutokana na
kesi ya uchochezi dhidi ya rais magufuli ambayo bado haijampatia dhamana hadi
sasa.
0 comments:
Post a Comment