John Banda, Bahi
Jordan Rugimbana |
MKUU wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana,
ameshangazwa na kitendo cha watumishi wote wa halmashauri ya Wilaya ya Bahi
kukosa ratiba ya utekelezaji wa mpango kazi.
Mshangao huo wa mkuu wa mkoa unakuja,
baada ya mkuu huyo kufanya ziara wilayani humo na kuanza kuzungumza na
watumishi hao ili kujua jinsi wanavyotekeleza mpango kazi wao.
Rugimbana alisema kuwa inashangaza kuona
watumishi hao hawana rariba ya utekelezaji wa mpango kazi wa maendeleo, akisema
kuwa wilaya hiyo haiwezi kufikia malengo yake kutokana na kazi kufanywa bila ratiba.
Mkuu huyo wa mkoa aliwauliza watumishi
hao kuwa mwenye ratiba hiyo anyooshe kidole amruhusu kwenda kuichukua ili kuwa
mfano kwa wengine.
Licha ya mkuu huyo kuuliza mwenye ratiba
ya kazi kunyoosha kidole lakini kulionekana kuwa kimya ishara yakuwa hakuna mwenye tariba hiyo.
"Kwa mtindo huu haiwezekani wilaya
hii kupata mafanikio ya utekelezaji miradi yake wakati hakuna hata mtumishi
mmoja ambaye anaratiba ya kazi
“Niwaambie ni muhimu kuwa na ratiba ya
mpango kazi wa maendeleo kwa kila mtumishi na kwa kufanya hivyo itarahisisha
utendaji wake", alisema.
Aidha aliwaahidi kurudi wilayani hapo
baadaye na kukagua tena mipango kazi, huku akisisitiza kuwa asingependa kuona watumishi
wa umma wanafanya mikutano isiyokuwa na tija.
0 comments:
Post a Comment