Mary Mtuka
Godfrey Simbeye |
TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)
imeingia makubaliano ya kuanzisha Baraza la Kibiashara na Uturuki kwa lengo la
kukuza biashara za hizo nchi mbili.
Makubaliano hayo yalifikiwa Dar es
Salaam juzi kwenye kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, alisema Baraza
hilo litaratibu juhudi za pamoja, kukusanya, kuunganisha, kuchambua, kuthamini
na kueneza taarifa zinazohusu biashara na ushirikiano kwenye uwekezaji.
Alisema Baraza litaanzisha na kukuza
viwanda, kupitia ushirikiano wa teknolojia wa mashirika na taasisi za kiuchumi
za Uturuki.
“Baraza litaandaa maonesho ya kibiashara
na kuhamasisha wanachama wake kushiriki na hatimae kuwezesha wajasiriamali wadogo na
wa kati kuwapa ujuzi na maarifa,” alisema Simbeye.
Aliongeza kuwa kutakuwa na ukusanyaji wa
takwimu na taarifa juu ya fursa za biashara na kusambaza taarifa kwa wanachama.
Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald
Mengi alisema wafanyabiashara na Watanzania wote wanatakiwa kuchangamkia fursa
hiyo kwa kuwa Uturuki ni mabingwa wa kilimo ambacho Watanzania wengi wanakitegemea.
Pia Mengi alimshukuru Rais John Magufuli
kwa kumleta nchini Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kwani kwa
wafanyabiashara ni fursa ya pekee ya kufungua milango ya biashara zao.
Hata hivyo, alisema kwa kushirikiana na
Baraza hilo litaunda kamati mbili, kila moja ikiwa na wajumbe wake na taasisi za kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment