Mwandishi Wetu, Morogoro
Sihaba Nkinga |
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha dawati la ulinzi na usalama katika
shule zote na kamati za ulinzi na usalama ngazi za kata na vijiji nchini kukabiliana
na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Sihaba
Nkinga, alisema hayo jana kwenye ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu ya Baraza
la Watoto la
Taifa cha siku mbili mjini hapa.
Aidha, aliwataka wajumbe wa kikao hicho
kujadili kwa kina ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na
kuwasilisha mapendekezo yao wizarani.
Aliongeza kuwa kutokana na kuzinduliwa
kwa mpango mkakati wa kupambana na kuzuia ukatili dhidi ya
wanawake na watoto
wa miaka mitano,
Serikali itahakikisha vitendo
vya ukatili vinapunguzwa kwa
asilimia 50 kupitia mpango kazi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo,
Caroline Augustino akizungumza na vyombo vya habari alisema Baraza hilo limefanya
ziara mikoani kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya redio na
runinga, ili jamii ifahamu maana na aina za ukatili dhidi ya watoto.
Caroline
aliwataka wasichana wa
umri mdogo kuachana
na tamaa zinazowafanya kujiingiza
kwenye matendo mabaya
yanayosababisha kukatisha ndoto
zao ikiwamo kushindwa kuendelea na masomo kwenye ndoa za utotoni na kutaka wazazi na walezi kutambua
kuwa mtoto wa kike ana fursa sawa na wa kiume hasa vijijini.
Pia alizitaka jamii za wafugaji na baadhi
za Kanda ya Ziwa kuacha tabia ya tohara mbili kwa watoto wa kiume na ukeketaji
kwa watoto wa kike kwani inasababisha vifo na maumivu ambayo yana athari mbaya za
kipindi kirefu.
0 comments:
Post a Comment