Mwandishi Wetu
SERIKALI imetoa tahadhari ya ugonjwa wa
mafua ya ndege, ikitaka wananachi kuzingatia kanuni za afya za kuzuia ugonjwa
huo.
Imetoa tahadhari hiyo kufuatia kubainika
uwepo wa virusi vya mafua makali ya ndege katika nchi jirani ya Uganda.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari na Waziri wa Afya, Jinsia, wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ilisema kuwa hadi
sasa ugonjwa wa mafua ya ndege haujaingia, lakini kuna haja ya kuchukua
tahadhari.
Ummy alisema ugonjwa huo uliosababishwa na
ndege pori, hauangalii mipaka, hivyo kunahitajika kuchukuliwa tahadharii
madhubuti ili kuzuia usiingie nchini.
"Wananchi wanatakiwa kuzingatia
kanuni za afya za kuzuia ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mara
moja wanapoona vifo vya ndege au kuku. Pia wanatakiwa kuripoti haraka kwenye
vituo vya kutolea huduma za afya mara wanapoona dalili zozote za ugonjwa
huu," alisema .
Hata hivyo alitaka wananchi kutojenga
hofu kuhusu ugonjwa huo, kwani haujaingia nchini, badala yake wajitahidi
kuudhibiti usiingie.
Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa maeneo
yalioathirika kuwepo kwa ugonjwa huo ni yanayozunguka Ziwa Victoria na ziwa
lenyewe, huku ikieleza kuwa umengundulika baada ya kuwepo kwa vifo vingi vya
ndege pori katika eneo ya Lutembe beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga na
Bukakata ya nchini Uganda.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo vifo hivyo
vimetokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata), huku ikihisiwa kuwa
ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege pori wanaohama
kutoka nchi za Ulaya.
"Vifo hivi vya ndege pori vilianza
kuonekana tangu Januari 2, mwaka huu na vimeonekana kuendelea hadi sasa, wakati
kwa hapa nchini hakuna vifo vya ndege vilivyoripotiwa hadi sasa," ilisema
taarifa hiyo.
Hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba hadi
sasa hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo nchini
Uganda, bado tunahitaji kuwa makini,” alisema
0 comments:
Post a Comment