Odace Rwimo, Uyui
Gabriel Mnyele |
MKUU wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora,
Gabriel Mnyele, amejiuzulu.
Mnyele ambaye ni Mwanasheruia kwa
taaluma jana alipita kila idara za Halmashauri ya Wilaya hiyo kuaga akianzia kwa
watumishi wa ofisi yake.
Taarifa za awali zilisema kuachia kwake
ngazi ya ukuu wa wilaya kulitokana na kutingwa na majukumu binafsi aliyonayo.
Aidha, imedaiwa kuwa Mkuu huyo aliandika
barua mwaka jana akiomba kujiuzulu nafasi hiyo.
Taarifa zaidi zilisema baada ya kuandika
barua alijibiwa na mamlaka ya uteuzi akikubaliwa kuachia nafasi hiyo.
Hata hivyo, Mnyele alipoulizwa jana
kuhusu taarifa hizo huku akicheka, alisema: “Mimi bado nipo ofisini na leo
nimehudhuria kikao cha ulinzi na usalama. Lakini kwa nini msiulize mamlaka ya
uteuzi?”
Baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo
ambao hawakutaka kutajwa majina walisema jana kuwa Mkuu huyo alipita kila idara
akianzia ofisi mwake kuaga.
“Bosi wetu alianzia ofisini kwake kuaga
watumishi na baadaye alipita kila idara na kubwa ambalo alikuwa akieleza ni
uamuzi alioufanya bila shinikizo,” alisema mmoja wao.
Alisema aliwambia uamuzi wa kusitisha
ajira yake hautokani na kushindwa kasi ya Rais Dk John Magufuli bali anataka
kufanya kazi zake binafsi.
“Alisema majukumu binafsi yamembana na
ndiyo maana kafikia uamuzi huo na si vinginevyo kama watu wanavyoweza kufikiria,”
alisema mtumishi huyo wa Halmashauri.
Aidha, inadaiwa aliwaeleza anaachia ili
wengine washike nafasi hiyo ila ataendelea kushirikiana na wana Uyui.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,
Hadija Makuwani alilieleza gazeti hili kuwa bosi wake huyo alimuaga asubuhi jana
kwa maelezo kuwa amesitisha ajira yake kwa hiari ili akafanye shughuli zake.
Aliongeza kuwa kwa sasa wanasubiri kuletewa
Mkuu mwingine wa Wilaya ili aendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea maendeleo
wananchi wao.
Gazeti hili lilimtafuta Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Aggrey Mwanri ili kupata maoni yake lakini simu yake ilikuwa
haipatikani muda wote hadi tunakwenda mtamboni.
0 comments:
Post a Comment