Emeresiana Athanas
TAASISI ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu
Muhimbili (Moi), imesema haina uhaba wa vifaa vya mazoezi ya viungo.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam
jana, Ofisa Uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi alisema taasisi hiyo haina uhaba na
kila mgonjwa hupewa matibabu kulingana na mahitaji.
Alisema wataalamu waliopo wanatoa
mazoezi ya viungo kwa njia mbalimbali ambazo ni huduma ya mikono kitaalamu na
vifaa vya mashine zinazotumia betri.
Mvungi alifafanua kuwa kitengo hicho cha
mazoezitiba hakijawahi kurudisha mgonjwa kwa kukosa vifaa, kwani wataalamu
wamejifunza njia mbalimbali za kutoa mazoezi kwa wateja wao.
"Tuna vifaa vya kutosha na
wataalamu wapo wa kutosha na wanatoa huduma mbalimbali, hatuna uhaba wa vifaa
na hatujawahi kurudisha mgonjwa au kuzidiwa kwa kukosa vifaa," alisema.
Mvungi aliwatoa hofu Watanzania na
kubainisha kuwa wataalamu hutoa mazoezitiba
kulingana na tatizo la mgonjwa anayefika hospitalini hapo.
0 comments:
Post a Comment