Mwandishi Wetu
Martha Mlata |
MBUNGE
wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata, anatuhumiwa
kutengua uamuzi wa Baraza la Madiwani la Novemba 28 mwaka jana na kuridhiwa na
Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Singida, kuhusu mahali makao makuu ya
wilaya hiyo yatakapojengwa.
Mlata
pamoja na kada mwingine wa CCM na Mbunge (Jina lake linahifadhiwa) wanatuhumiwa
kuingilia utendaji na kutengua uamuzi halali
wa madiwani.
Akizungumza
na mwandishi wa gazeti hili jana, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida,
Naruma Hanje alisema Mlata amekuwa haridhiki na nafasi aliyonayo, kwani anataka
kuwa Mwenyekiti wa Mkoa na wa Wilaya zote, ili afanye uamuzi bila maelekezo kutoka
kwa wenyeviti wa wilaya.
“Mimi
nimesikia ameagiza niwaandikie barua madiwani ambao hawakuhudhuria mkutano wake
wajieleze, lakini siwezi kufanya hivyo kwa kuwa hawana kosa, wanafanya kazi na
waliamua eneo la kujenga Halmashauri kwa kikao halali kisheria, Mlata analeta
vurugu tu,” alisema Hanje.
“CCM
tuna utaratibu wetu, mtu akikosea huitwa kuonywa, lakini Mlata alifika Ilongero
na (Mbunge) na kutoa matusi hadharani, hawa ni watoto wetu tumewalea,
wametuvunjia heshima kabisa,” alisema.
Mwenyekiti
wa Halmashauri hiyo, Elia Digha alipopigiwa simu kuulizwa kama ana taarifa ya
jambo hilo alisema: “Najua na naamini madiwani hawakukosea, walifuata sheria,
kinachofanywa na Mlata na … ni kujitoa ufahamu kwa jambo ambalo liko wazi.”
Alisema
Serikali inawataka wajenge Halmashauri kwenye maeneo ya wazi ambako hawatatumia
fedha nyingi kulipa fidia, lakini Mlata na mwenzake wamekuwa wakishirikiana na
kikundi kidogo ambacho hata si sehemu ya madiwani kufanyia fujo madiwani.
Alisema
baada ya kina Mlata kufika Ilongero Januari 7, waliwatangazia wananchi kuwa
eneo hilo litakuwa wilaya kabla halijatangazwa kisheria na matokeo yake
waliwaondoa kwa nguvu viongozi wa CCM wa wilaya kwenye jengo la Singida mjini bila
makubaliano.
Digha
alifafanua kuwa Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya hiyo chini ya Hanje, ilipewa
mapendekezo na wataalamu juu ya umuhimu wa kujenga makazi hayo Kinyamwambo
badala ya Ilongero na ikakubaliana kwa sababu za kiuchumi.
Mwenyekiti
huyo alisema Oktoba 20, 2014 katika muhtasari namba 42/2014, wa Baraza la Madiwani
chini ya Juma Samwi, Diwani wa zamani wa Ilongero alihudhuria.
“Sisi
madiwani tulifuata taratibu na sheria, Mkuu wa Mkoa aliyeondoka alikuwa hafuati
sheria, anatuvuruga, anakivuruga chama chetu sababu maazimio haya ya madiwani
yalikubaliwa pia na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya, Septemba 28 mwaka jana, kikao
cha kamati ya uongozi kiliridhia, kikifuatiwa na kikao cha kamati ya kudumu ya
uchumi na fedha cha Novemba 13 ambacho kilitoa mapendekezo kwenye Baraza,”
alisema Digha.
“Hata
kamati ya chama ya madiwani wa CCM ilikubali, na kikao hicho kilikuwa na
madiwani 29 na wote waliridhia, hadi kupelekea Baraza halali la madiwani Oktoba
28 mwaka jana kupitisha maazimio kuwa makao makuu yajengwe Kinyamwambo badala
ya Ilongero,” alisema.
Akijibu
tuhuma hizo Mlata alisema hazina ukweli na kuwa wanaomtangazia sifa mbaya
wataumbuka kutokana na kukosa hoja za msingi.
“Waambie
wafuate taratibu za chama, kufikisha malalamiko yao wanatakiwa kutambua kuwa
mimi ni bosi wao kichama, hivyo siko tayari kuona ukiukwaji unatokea
nikanyamaza,” alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema wanaolalamika ndio wavunja nchi na wanapaswa ‘kutumbuliwa’, kwa
kuwa ni ‘majipu’ kwenye mkoa na wilaya hiyo ambayo ipo kwenye mchakato wa
kupiga hatua za kimaendeleo.
Alisema
kwa upande wake hana maslahi yoyote anayopigania katika suala hilo, hivyo ni
jambo la kusikitisha yeye kuhusishwa.
0 comments:
Post a Comment