Mwandishi Wetu
Japhary Michael |
MBUNGE wa Moshi Mjini, Japhary Michael,
ameeleza kusikitishwa kwake juu ya maofisa usalama kuwazuia yeye na Meya wa Manispaa
hiyo kuingia Ikulu ndogo ya Moshi kuhudhuria kikao cha Rais John Magufuli na viongozi
wa dini.
Michael ambaye ni wa Chadema, alisema
tukio hilo lilitokea juzi baada ya kufika Ikulu kutokana na mwaliko wa Mkurugenzi
wa Manispaa ya Moshi kushiriki kikao hicho.
Mbunge huyo alisema aliitika mwaliko huo
lakini ghafla akiwa kwenye foleni yeye na Meya wakazuiwa kuingia na kutakiwa warudi
walikotoka.
Alisema alifika eneo la tukio saa 6.30
mchana akamkuta Mstahiki Meya akiwa ametangulia kwenye foleni.
“Tulipata mwaliko na tukaheshimu, ila
katika mazingira ambayo hayaeleweki tulizuiwa na watu wa usalama na sisi
hatukuhitaji kugoma tukaondoka,” alisema.
Alisema jmbo la kusikitisha wakati akiwa
kwenye foleni na viongozi wa dini, viongozi wa CCM na watendaji wengine wa Serikali,
alichomolewa yeye na Mstahiki Meya wakiambiwa hawastahili kushiriki kika hicho.
Alisema Mkurugenzi alijaribu kuwatetea
kwa kuwambia ndiye aliyewapa mwaliko kwa maelekezo ya Katibu Tawala wa Mkoa,
hakusikilizwa kabisa.
“Mimi mbunge sijaumizwa, kwa kuwa
nimetimuliwa bali ninasikitika kwa kuwa tunatiwa woga wa kushiriki shughuli za
viongozi wetu wa kitaifa hasa wanapofanya ziara katika maeneo tunayowakilisha,”
alisema.
Alisema kutokana na tukio hilo, huenda
jamii ikawajengea taswira mbaya kwamba hawaheshimu viongozi wa kitaifa pale
wasiposhiriki matukio mengine.
“Mimi binafsi nimetafsiri tukio hilo
lililonipata kama ubaguzi wa kiitikadi kwa mambo ambayo ni ya kitaifa,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment