Hussein Ndubikile
CHUO Kikuu cha Kampala (KIU), tawi la Dar es Salaam
kimesema ujenzi wa hospitali yake ya rufaa unatarajiwa kukamilika Oktoba.
Awali ujenzi huo ulikuwa ukamilike Juni ila kutokana na kutokamilika
kwa taratibu ulisogezwa mbele.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Masoko wa
KIU, Rashid Noor alisema ujenzi umefikia hatua nzuri na kinachofanyika sasa ni
umaliziaji wa maeneo ya ndani ya jengo.
“Mafundi sasa wanamalizia eneo la ndani ya jengo na mambo
yakienda vizuri tunatarajia itafunguliwa muda uliopangwa,” alisema Rashid.
Alisema vifaa vinavyohitajika kwa mafunzo na matibabu
vimeshawasili huku akiongeza kuwa kukamilika kwake kutasaidia watu wa karibu na
chuo hicho kupata huduma bora ya afya.
Alisisitiza kuwa madaktari wa hospitali hiyo watatoka
ndani na nje ya nchi zinazoshirikiana na chuo hicho.
Aliongeza kuwa wanafunzi wanaosomea vitivo vya Sayansi
watafanyia humo mazoezi ya vitendo ili kuendana na maelekezo ya Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia, yanayotaka chuo kinachofundisha taaluma ya
udaktari kuwa na hospitali yenye hadhi hiyo.
Aidha, alisema jengo hilo linatarajiwa kufunguliwa na
Mkuu wa Chuo hicho, Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.
0 comments:
Post a Comment