Mwandishi Wetu
UHABA wa vyoo, vifaa vya kufundishia na walimu wasio na
sifa ni moja ya changamoto inayotajwa kurudisha nyuma jitihada za kuinua sekta
ya elimu katika wilaya Kisarawe mkoani Pwani.
Ofisa Elimu Msingi wa Kisarawe, Omari Bane amesema changamoto
hizo zimesababisha utoro kwa baadhi ya wanafunzi, hivyo kupunguza idadi ya
wanafunzi wanaohudhuria masomo.
Bane alisema tatizo la vyoo husababisha baadhi ya
wanafunzi kuwa watoro kwa sababu baadhi ya wanafunzi huishi mbali na shule.
"Changamoto hizi pia huwakumba walimu waliokosa
nyumba za kuishi ambao wanaishi mbali na maeneo ya shule na hivyo hukosa muda
wa kuwasadia wanafunzi kwa kukosa muda na kulazimika kuwahi majumbani kwao
"alisema Bane
Kuhusu walimu wasio na sifa, alisema ameishukuru Serikali
kwa kazi ya kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma hasa walimu wa shule za msingi,
kwani walimu hao wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa jitihada za
kuinua kiwango cha elimu.
Alisema zoezi hilo la kuondosha walimu limeleta pengo
kubwa kwa Wilaya na kuongeza kuwa idadi ya uhitaji wao sasa inafikia 80.
Bane alisema kauli mbiu ya kusoma na kuandika ni
msingi wa maendeleo ya Taifa itakwenda sambamba na uhalisia uliopo baada ya
kuondoa walimu wasiokuwa na sifa.
Diwani wa Kata ya Kisarawe Abel Mudo alisema utoaji
wa zawadi kwa wanafunzi bora na walimu mara kwa mara itaongeza chachu na
juhudi katika masomo na kuleta msukumo wa ushindani katika taaluma na hivyo
kuwafanya wale wavivu waweze kuingia kwenye ushindani na kubadilika.
Mulo alisema ni vyema walimu waliobaki mashuleni kufanya
kazi hiyo ya ufundishaji kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu
katika Wilaya na kuinua maendeleo ya elimu na kupunguza umasikini.
Katika sakata la vyeti feki kuna jumla ya watumishi 11 mpaka leo wamekata rufaa kwa kupinga zoezi hilo
0 comments:
Post a Comment