Abraham Ntambara
Rais John Magufuli |
RAIS John Magufuli leo anatarajia
kumkabidhi Rais Yoweri Museveni wa Uganda uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) katika mkutano wa wakuu wa nchi za EAC unaofanyika Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda, Dk Augustine Mahiga alisema hayo juzi alipozungumza
na vyombo vya habari, baada ya ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa EAC.
Alisema vikao vya wakuu wa nchi wanachama
hufanyika mara mbili kwa mwaka, wakati vingine vikiwamo vya mawaziri hufanyika
zaidi ya mara mbili, ili kupima na kutathmini mwelekeo wa ushirikiano wa nchi
hizo.
“Katika vikao vya marais huwa na nchi Mwenyekiti,
ambaye sasa ni Tanzania, kwa miaka miwili mfululizo, lakini sasa tumemaliza
muda wetu na katika kikao hiki cha 18 cha marais, Rais Magufuli atamkabidhi
uenyekiti Rais Museveni,” alisema Dk Mahiga.
Alifafanua kuwa kwa mwaka uliopita hadi
Aprili, yeye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa EAC na kutokana na
muda kwisha, katika mkutano wa mwisho wa mawaziri uliofanyika Arusha,
alimkabidhi uenyekiti Waziri wa Uganda.
Kwa mujibu wa Dk Mahiga, ikiwa mwenyekiti
wa EAC Tanzania ilifanya mambo kadhaa katika kuboresha uhusiano wa wanajumuiya,
ukiwapo ujio wa Sudani Kusini ambayo uanachama wake, ulikamilika chini ya
uenyekiti wa Tanzania.
Katika mkutano wa sasa, Dk Mahiga alisema
kutakuwa na masuala mbalimbali yatakayozungumzwa na kutolewa uamuzi na marais.
Miongoni mwao ni pamoja na ripoti ya ushirikiano
ya miaka miwili iliyopita chini ya uongozi wa Tanzania, ambayo itazingatia
sekta muhimu za kiuchumi za biashara, uwekezaji na huduma za kuendesha nchi.
0 comments:
Post a Comment